
Mambo ya kufanya ili kupata mimba haraka
Mnapokuwa tayari kuanzisha familia jitihada hufanyika ili wanamke kushika mimba.
Ila Kuna baadhi hupitia changaoto ya kuchelewa kupata ujauzitio kwa muda mrefu licha ya jitihada nyingi wanazozifanya.
Kuna baadhi ya mambo yaliyothibitishwa na wataalamu mwanamke akiyafanya au akiyazingatia humsaidia kupata mimba kwa haraka na kukua bila changaoto.
Mambo hayo ni kama vile:
Kufanya checkup:
Muda ambao upo tayari kubeba mimba ni muhimu kufanya kwanza checkup kujua hali ya afya yako kwanza.
Pia ni muhimu kutumia vidonge ya vitamin hasa vidonge vya folic acid ambayo vinasaidia kumkinga mtoto na matatizo ya
kuzaliwa nayo hasa katika wiki za mwanzo za ujauzito.
Na kama una matatizo yoyote ya kiafya ni muhimu kupata matibabu kwanza kabla ya kubeba mimba.
Fuatilia na uulewe vizuri mzunguko wako wa hedhi:
Jambo lingine la kuzingatia ni kujua mzunguko wako wa hedhi na kuuelewa vizuri, hii itakusaidia kujua ni muda gani yai
limekomaa na lipo tayari kurutubishwa kutunga mimba.
Muda huo ukiujua ni muda mzuri wa kufanya tendo la ndoa ili kurutubisha yai kwa wakati sahihi.
Baki kitandani kwa muda mara baada ya kumaliza kufanya tendo:
Ili kuongeza uwezekano wa kupata mimba haraka inashauriwa mwanamke kubaki amelala kitandani kwa muda kati ya dakika 10 mpaka 15
baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa.
Muda huo ni makadirio ya muda ambao mbegu za kiume zitakuwa zimeishaingia kwenye shingo ya kizazi kuelekea kulitafuta yai.
Punguza msongo wa mawazo:
Msongo wa mawazo ni tatizo la kiafya ambalo pia linaweza kusababisha matatizo mengine ya kiafya mwilini.
Msongo wa mawazo pia unaweza kusababisha kupunguza uwezo wa wanamke kushika mimba haraka.
Jitahidi kupunguza msongo wa mawazo inasaidia kuongeza uwezo wa kushika mimba haraka.
Jali afya yako:
Kufanya mazoezi mara kwa mara ni moja ya njia kuimarisha mwili na kuimarisha afya yako.
Fanya mazoezi kwa kiasi kwasababu kuna baadhi ya tafiti zinaonesha kuwa kufanya mazoezi magumu sana kunasababisha
kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi kwa mwanamke.
Acha kuvuta sigara kama ni mvutaji, tafiti zinaonesha uvutaji wa sigara unachangia kwa kiasi kikubwa wanamke kuchelewa kubeba mimba.
Unaweza pia kusoma: