Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Maumivu ya tumbo kwa mjamzito

Maumivu ya tumbo kipindi cha ujauzito mara nyingi huwa ni hali ya kawaida tu kwa mjamzito, ila inaweza kuwa hali ya kuogopesha pia.
Mara nyingi maumivu ya tumbo wiki 12 za mwanzoni za ujauzito ni kawaida kwasbabu ya mabadiliko ya homoni kwa mjamzito na kutanuka kwa mfuko wa kizazi.
Kuna muda maumivu hayo huwa makali na ya kuchoma na mengine huwa ya kawaida.
Jambo gumu kwa wajawazito ni kuweza kutambua kama maumivu hayo ni makali sana au ni ya kawaida.
Ni muhimu kujua ni kama ni maumivu ya kawaida au kama maumivu ni makali sana ili uwahi kumuona daktari.

Kuna aina tofauti tofati za maumivu ya tumbo kipindi cha ujauzito kama ifuatavyo:

Maumivu ya gesi kwa mjamzito:
Maumivu ya gesi tumboni kwa mjamzito husababishwa na tumbo kujaa gesi, yanaweza kuwa maumivu upande mmoja au yanayosambaa tumboni kote, mgongoni na kwenye kifua.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali mjamzito husumbuliwa sana na tumbo kujaa gesi kwasababu ya ongezeko la homoni ya progesterone kipindi cha ujauzito.
Pia kwasababu ya mgandamizo wa kizazi kwenye utumbo.

Maumivu ya kutanuka kwa misuli ya nyonga:
Mimba inavyokuwa kubwa misuli ya nyonga nayo hutanuka ili kuweza kuhimili ukubwa na uzito wa mtoto tumboni.
Hali hiyo ya kutanuka kwa misuli ya nyonga kwa mjamzito humsababishia maumivu ya tumbo, nyonga na kwenye kinena.

Maumivu kwasababu ya choo kigumu:
Kupata choo kigumu ni moja ya tatizo la mara kwa mara kwa wajawazito wengi.
Vitu kama vile mabadiliko ya homoni kwa mjamzito, kula vyakula vyenye uhaba wa nyuzi lishe na maji, kutofanya mazoezi, vidoge vya madini chuma na kuwa na wasiwasi kunaweza kusababisha kupata choo kigumu.
Kuwa na Choo kigumu wakati mwingine kunaweza kusababisha maumivu makali ya tumbo kwa mjamzito.

Maumivu kwasababu ya kujimbinya kwa misuli ya mfuko wa kizazi:
Ni hali ya kawaida hutokea kwa mjamzito misuli ya mfuko wa kizazi kujiminya kusababisha hali kama uchungu lakini si uchungu wa kweli.
Hali hiyo husababisha maumivu kwa mjamzito ila maumivu hayo huisha baada ya muda mchache.

Hayo yote ni maumivu mbalimbali ya tumbo ya kawaida kwa wajawazito.

Ila unapohisi maumivu makali ya tumbo au maumivu ya tumbo yaliyoambatana na dalili kama vile:
- Homa kali.
- Maumivu wakati wa kukojo.
- Maumivu ya kichwa.
- Uchovu kuliko kawaida.
- Kichefuchefu na kutapika.
- Kuona maluweluwe.
- Kuvimba sehemu za mwili.
- Na kutoka damu au uchafu sehemu za siri.
Ni vizuri kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.

0
0