
Faida ya Kula Giligilani Kiafya
Giligilani ni aina ya mmea unaotumika kama kiungo cha chakula kwa ladha yake ya uchachu.
Ni mmea mlaini na kila sehemu ya mti huu inalika, ila kwa asilimia kubwa majani yake na mbegu zake ndizo hutumika.
Si tu kuongeza ladha pia giligilani ina virutubisho muhimu kwa afya ya binadamu.
Baada ya tafiti mbalimbali za kisayansi mmea huu wa giligilani umeonekana kuwa na faida zifuatazo kwa afya ya binadamu.
Husaidia kushusha sukari kwenye damu.
Kuwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu ni moja kati ya vihatarishi vya mtu kupata kisukari aina ya pili.
Giligilani inasaidia kwa kiasi kikubwa kushusha kiwango cha sukari kwenye damu.
Na kama una tatizo la kupungukiwa na sukari mwilini au kama unatumia dawa za kisukari kushusha sukari,
haishauriwi kutumia giligilani kwasaabu inaweza kusababisha sukari kushuka zaidi ya kawaida.
Inasaidia kusafisha mwili na kuongeza kinga ya mwili.
Virutubisho vya giligiani vinasaidia kusafisha mwili na kuzilinda seli za mwili zisidhulike kirahisi,
pia inasaidia kuongeza kinga ya mwili na uwezo wa mwili kupambana na magonjwa mbalimbali.
Kinga dhidi ya saratani.
Utafiti mmoja wa maabara ulifanikiwa kugundua kuwa virutubisho vya giligillani vinaweza kudhibiti
ukuaji wa seli za saratani ya mapafu, tezi dume, matiti na saratani ya utumbo mpana.
Inasaidia kulinda mishipa ya fahamu na kuimarisha afya ya ubongo.
Virutubisho vya giligilani husaidia kusafisha mwili na kuzilinda seli za mwili zikiwa ni pamoja na seli za ubongo na mishipa ya fahamu.
Itakusaidia kuimarisha afya yako ya ubongo, uwezo wako wa kufikiri na kutunza kumbukumbu.
Na kwa wazee ni kinga ya magonjwa ya uzeeni yanayosababishwa na kufa kwa seli za ubongo kama vile kupoteza
kumbukumbu na ugonjwa wa kutetemeka (Parkinson’s Disease).
Pia giligilani inaweza kuwa ni msaada kwa watu wenye wasiwasi uliopitiliza.
Inasaidia kuimarisha afya ya ngozi.
Kutokana na uwezo wa virutubisho vya giligilani kusafisha mwili na kuzikinga seli za mwili,
pia seli za ngozi zinalindwa zisiharibiwe na mwanga wa jua na kuzuia dalili za uzee,
kama vile mikunjo ya ngozi kuonekana mapema.
Insaidia kuimarisha afya ya moyo.
Tafiti mbalimbali za maabara na kwa wanyama zimegundua kuwa virutubisho kwenye giligilani
vinasaidia kuondoa vihatarishi vya magonjwa ya moyo kama vile kupanda kwa shinikizo la damu na
kuongezeka kwa mafuta mabaya ya cholesterol.
Giligilani inasaidia kutibu matatizo kadhaa ya tumbo, maumivu ya tumbo, tumbo kujaa gesi na pia inasaidia kuongeza hamu ya kula.
Virutubisho vya giligilani pia vimeonekana kuwa na uwezo wa kupambana na baadhi ya bakteria wanaosababisha magonjwa ya tumbo.
Pia kuna utafiti mwingine wa maabara ulionesha kuwa virutubisho vya giligilani vinaweza kudhibiti baadhi ya bakteria wanaosababisha mkojo mchafu (U.T.I).
Unaweza pia kusoma: