Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Faida za kunywa chai ya kijani kiafya

Chai ya kijani ni aina ya chai ambayo huandaliwa kwa kutumia majani ya chai ambayo huchumwa moja kwa moja kutoka kwenye mti wa chai kabla ya kuchakatwa kiwandani.
Asili ya chai ya kijani ni china licha ya kutumiwa kama kinywaji pia chai ya kijani imeonekana kuwa na virutubisho vingi muhimu kwa afya kuliko chai ya kawaida nyeusi.
Chai ya kijani imetanjwa na wataalamu mbalimbali kuwa ni moja kati ya kinywaji vyenye faida nyingi za kiafya.
Katika makala hii tuzifahamu faida mbalimbali za kiafya ambazo mtu anaweza kuzipata kwa kunywa chai ya kijani.

Husaidia kuimarisha afya ya ubongo:
Chai ya kijani ina virutubisho muhimu kwa afya ya ubongo, virutubisho ambayo husaidia kuchangamsha ubongo.
Pia virutubisho kwenye chai ya kijani vinasaidia kumuondolea mtu wasiwasi, vinasaidia kumpa mtu mood nzuri, kuongeza umakini na kuongeza uwezo wa kutunza kumbukumbu.
Watu wengi waliojaribisha kutumia chai ya kijani na kahawa walisema chai ya kijani imewapa nguvu na kuongeza ufanisi wao wa kazi kuliko kahawa.

Inachochea uyeyushaji wa mafuta mwilini:
Kama unapanga kupunguza uzito basi hakikisha kwenye mlo wako wa siku usikose kunywa chai ya kijani.
Baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa chai ya kijani ina uwezo wa kuongeza uyeyushaji wa mafuta mwilini.

Husaidia kupunguza hatari ya kupata saratani:
Mkusanyiko wa sumu ndani ya mwili unaweza kusababisha magonjwa ya muda mrefu kama vile saratani.
Chai ya kijani ina viondoa sumu mbalimbali ambavyo vinasaidia kuondoa sumu ndani ya mwili.
Tafiti mbalimbali zimeonesha kuna mahusiano kati ya virutubisho vya chai ya kijani na kupunguza hatari ya kupata saratani sehemu mbalimbali mwilini.
Saratani ya matiti, saratani ya tezi dume na saratani ya utumbo mpana ni baadhi ya saratani ambazo zinaweza kuzuilika kwa unywaji wa chai ya kijani.

Husaidia kuzuia ubongo kuzeeka:
Kwa watu waliokula chumvi nyingi husumbuliwa na matatizo ya uzeeni kama kupoteza kumbukumbu na tatizo la kutetemeka ambayo yanasababishwa na kuzeeka kwa ubongo.
Unywaji wa chai ya kijani unasaidia kuukinga ubongo usizeeke na kumkinga mzee na matatizo hayo ya uzeeni.

Husaidia kupunguza harufu mbaya mdomoni:
Virutubisho kwenye chai ya kijani pia vinasaidia kuimarisha afya ya kinywa.
Virutubisho hivyo huzuia ukuaji wa bacteria kinywani hasa bacteria wanaosababisha ukungu kwenye meno na kuoza meno.

Kinga dhidi ya kisukari aina ya 2:
Utafiti uliofanyika nchini japan kwa watu waliokuwa wanatumia chai ya kijani mara kwa mara walionekana kupunguza asilimia 42 ya hatari ya kupata kisukari aina ya 2.
Na tafiti zimeonesha chai ya kijani inasaidia kuimarisha utendaji kazi wa homoni ya insulin pamoja na kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu.

Kinga dhidi ya magonjwa ya moyo:
Tafiti zimeonesha kuwa chai ya kijani inaweza kusaidia kuondoa viatarishi vya magonjwa ya moyo kama vile mafuta mabaya ya cholesterol ambayo yanaweza kuganda kwenye mishipa ya damu.
Chai ya kijani inaweza kuondoa mafuta hayo, kuifanya damu kupita kwa wepesi kwenye mishipa ya damu na bila kuleta shida kwenye moyo.

Husaidia kupunguza uvimbe kwenye kizazi.
Tafiti zimeonesha kuwa unywaji wa chai ya kijani kwa wanawake inaweza kusaidia kupunguza ukubwa au inadi ya vimbe kwenye kizazi kama ana tatizo hilo.

0
0