
Kabla ya kula kitunguu maji zingatia mambo haya
Moja kati ya viungo maarufu vya chakula ni kitunguu maji.
Kitunguu hiki mbali na kusaidia kuongeza ladha ya chakula pia kina virutubisho mbalimbali muhimu kwa afya ya binadamu.
Kitunguu maji kina wingi vitamin C, vitamin muhimu kwa kuimarisha kinga ya mwili, kuimarisha na kuzalisha tishu za mwili
pia husaidia kufyonza madini chuma mwilini kwaajili ya uzalishaji wa seli nyekundu za damu.
Kitunguu maji kina faida hizi kwa afya ya binadamu.
1. Kitunguu maji husaidia kuimarisha afya ya moyo, pia husaidia kupunguza mafuta ya cholesterol mwilini ambayo huhatarisha afya ya moyo.
2. Kitunguu maji kina virutubisho ambavyo husaidia kukukinga na saratani mwilini.
3. Kitunguu maji husaidia kushusha kiwango cha sukari kwenye damu.
4. Kitunguu maji husaidia kuimarisha afya ya mifupa.
5. Kitunguu maji husaidia kuimarisha afya ya mfumo wa chakula.
6. Pia kuna faida nyingine nyingi ambazo unaweza kuzipata kwa kutumia kitunguu maji.
Ila kabla ya kutumia kitunguu saumu ni muhimu kufahamu mambo haya:
Ulaji wa kitunguu maji unaweza kusababisha matatizo ya tumbo kwa baadhi ya watu kama vile maumivu ya tumbo,
mvurugiko wa tumbo au tumbo kujaa gesi.
Kuna baadhi ya watu wana allergy na kitunguu maji, ikiwa utakula kitunguu maji na kupata dalili zozote za mzio au allergy
kama vile kuwashwa au kutoka vipele sehemu mbalimbali za mwili ni vizuri ukaacha utumia kitunguu maji na kumuona daktari.
Kumbuka kuwa kitunguu maji hutoa kemikali ambazo husababisha macho kuwasha waati mwingine kukusababishia kutoa macho.
Ili kujikinga na tatizo hilo kabla ya kukata kitunguu maji kimenye na ukioshe kwenye maji yanayotiririka, au unaweza
kuwasha jinti yakiberiti ukiwa unakata kitunguu maji itasaidia kupunguza gesi hiyo inayosababisha macho kuwasha.
Kitunguu maji pia kinaweza kusababisha kiungulia kwa baadhi ya watu.
Vile vile kitunguu maji kinaweza kusababisha harufu mbaya mdomoni.
Pia kitunguu maji kina kemikali ambazo zinaweza kuzuia damu kuganda mwilini.
Hivyo haishauriwi kutumia kitunguu maji kwa wingi kama unataka kufanyiwa upasuaji au kama unataka kuingia leba
kwasababu kinaweza kusababisha damu kushindwa kuganda kwa wakati na kusababisha kupoteza damu nyingi.
Pia kama unatumia dawa za kuzuia damu kuganda ni vizuri kupata ushauri wa daktari kabla ya kutumia kitunguu maji.
Unaweza pia kusoma: