
Vyakula vya Kuimarisha Afya ya Ubongo na Afya ya Akili
Ubongo ni kiungo muhimu mwilini, kinaratibu matendo yote ya mwili, matendo ya hiari na yasiyo ya hiari.
Ubongo kama viungo vingine vya mwili unahitaji virutubisho kutoka kwenye vyakula mbalimbali ili kufanya kazi zake vizuri.
Kwa mujibu watafiti mbalimbali za kisayansi hivi ni baadhi ya vyakula vinavyosaidia kuimarisha afya yako ya ubongo na uwezo wa kutunza kumbukumbu.
Samaki wa Mafuta:
Salmoni, Samaki jamii ya bangala, dagaa wa maji chumvi, Sardini na Heringi hao ni baadhi ya samaki wa maji chumvi.
Tafiti zimeonesha kuwa wana wingi wa mafuta hasa aina ya omega-3, mafuta ambayo kwa asilimia kubwa yanaunda tishu za ubongo.
Mafuta hayo yanasaidia kuimarisha afya ya ubongo na kuongeza uwezo wa ubongo kutunza kumbukumbu.
Kahawa:
Kahawa ina wingi wa caffeine na viondoa sumu.
Viondoa sumu vinasaidia kuondoa kemikali hatari mwilini na kuzilinda seli za ubongo zisiharibiwe na kemikali hizo.
Caffeine inasaidia kuongeza umakini kwa kuzuia homoni zinazoweza kukufanya uhisi usingizi.
Pia caffeine inasaidia kuongeza homoni zinazokufanya kuwa na mood nzuri.
Unywaji wa kahawa mara kwa mara hasa kwa watu wazima wanaokunywa vikombe 3 mpaka 4 kwa siku,
umeonekana kusaidia kupunguza hatari ya kupata matatizo kwenye mfumo wa fahamu kama vile ugonjwa wa kutetemeka na kupoteza kumbukumbu.
Binzari manjano:
Binzari manjano virutubisho vyake vina uwezo wa kupita moja kwa moja kuingia kwenye ubongo inasaidia kuondoa kemikali hatari na kuzilinda seli za ubongo.
Vinasaidia katika uzalishaji wa seli mpya za ubongo, vinasaidia kupunguza msongo wa mawazo pia vinasaidia kuongeza uwezo wa ubongo kutunza kumbukumbu.
Mbegu za maboga:
Mbegu za maboga zina wingi wa viondoa sumu, zinasaidia kusafisha mwili na kuzilinda seli za ubongo.
Pia mbegu hizi zina wingi wa madini ya magnesium, shaba na chuma madini ambayo yanasaidia kuongeza kinga kwenye ubongo,
kuimarisha utendaji kazi wa ubongo, na kuongeza uwezo wa ubongo kujifunza na kutunza kumbukumbu.
Karanga:
Karanga, korosho, mlozi na jamii nyingine kama hizo za karanga tafiti zimeonesha kuwa zina msaada katika kuimarisha afya ya moyo.
Kuimarika kwa afya ya moyo kuna uhusiano na kuimarika kwa afya ya Ubongo na kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya akili.
Uwepo wa mafuta safi, viondoa sumu na vitamin E kwenye karanga vimeonekana kusaidia kuimarisha afya ya ubongo.
Machungwa:
Nusu kipande tu cha chungwa ukila kwa siku kinatosha kuupatia mwili wako vitamin C yote inayohitajika mwilini kwa siku.
Baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa uwepo wa vitamin C kwa wingi kwenye damu unasaidia kuimarisha uwezo wa ubongo kufanya
kazi kama vile kuongeza umakini, kuongeza uwezo wa kutunza kumbukumbu na kuongeza uwezo wa kufanya maamuzi kwa haraka.
Mayai:
Mayai ni moja ya chakula chenye wingi wa virutubisho muhimu kwa afya ya ubongo.
Kiasi cha mayai 2 kwa siku kinatosha kuupatia mwili kiwango cha virutubisho hivyo kinachohitajika mwilini.
Virutubisho hivyo vimeonekana kusaidia kuimarisha uwezo wa ubongo kufanya kazi na kutunza kumbukumbu.
Chai ya kijani:
Chai ya kijani nayo ina wingi wa caffeine ambayo inasaidia kuimarisha utendaji kazi wa ubongo, kukuongezea umakini na uwezo wa kutunza kumbukumbu.
Chai ya kijani pia ina virutubisho vingine vinavyosaidia kuzilinda seli za ubongo na kukufanya kuwa na utulivu wa akili.
Pia chai ya kijani inasaidia kuimarisha uwezo wa ubongo kutunza kumbukumbu.
Unaweza pia kusoma: