Muonekano wa Giza:

Msaada

Picha inaonesha mkono wa mwanamke akiwa ameshika uteute katikati ya vidole vyake viwili.

Kutokwa na Uchafu/Harufu sehemu za Siri kwa Mwanamke, Ni Ishara ya nini?

Ni hali ya kawaida kwa mwanamke kutoka majimaji ukeni kwasababu mbalimbali za kiafya kwa wanawake.

Majimaji hayo yanasaidia kuweka uke safi na kumkinga mwanamke dhidi ya maambukizi ya magonjwa mbalimbali ukeni.

Majimaji hayo hutofautiana kwa rangi, muonekano wake na kiwango kinachotoka ukeni na inategemeana na umri wa mwanake na wakati wa hedhi.

Unapoona mabadiliko yoyote kwenye majimaji hayo yanayotoka ukeni inaweza kuwa ni ishara ya ugongwa.

Mabadiliko hayo yanaweza kuwa rangi au harufu ya majimaji hayo yanayotoka ukeni.

Ni muhimu kufahamu utofauti huo uliopo kwenye majimaji ya ukeni kama ni kawaida au si hali ya kawaida.

Katika makala hii tufahamu kuhusu utofauti uliopo kwenye majimaji ya ukeni ili kujua kama ni hali ya kawaida au si hali ya kawaida.

Uteute mweupe mzito:

Uteute mweupe mzito na unaonata ila usiotoa harufu kali ni hali ya kawaida kwa mwanamke hasa mwanzoni au mwishoni mwa hedhi.

Uteute msafi na mwepesi kama maji:

Kwa mwanamke anapokuwa katikati ya mzunguko wake wa hedhi hasa muda ambao yai hushuka kwaajili ya kutunga mimba ni kawaida kuona ukeni unatoka uteute msafi na mwepesi kama maji.

Uteute msafi na unaonata:

Endapo ukeni utatoka uteute mzito, msafi na unaonata ambao si mwepesi kama maji ni ishara ya kuwa upo kwenye siku za hatari endapo utashiriki tendo la ndoa una uwezekano mkubwa wa kupata mimba.

Uteute wa rangi ya kahawia au nyekundu:

Uteute wa aina hii huonekana kipindi cha hedhi au mara baada ya kumaliza hedhi, pia kuna muda ambao mwanamke anaweza kuiona katikati ya mzunguko wake wa hedhi.

Ni kwasababu inaweza kutokea vidone vya damu kutoka katikati ya mzunguko wa hedhi hasa siku za hatari kwa mwanake.
Muda mwingine hali hiyo huwa ni ishara ya mimba changa kama umetoka kushiriki tendo la ndoa siku zako za hatari.

Uteute wa njano au wa kijani:

Uteute wa njano iliyokoza au kijani inaweza kuwa ni ishara ya magonjwa kwenye viungo vya uzazi kwa mwanake hasahasa ukiwa ni uteute mzito na unaotoa harufu mbaya.

Ukiona hali hiyo ni vizuri kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.

Muda mwingine unjano kwenye uteute inaweza kuwa kawaida kwasababu ukikaa kwenye hewa muda mrefu unabadilika rangi.

0
0
1