Muonekano wa Giza:

Msaada

Picha inamuonesha mwanamke akiwa ameinama na kushikilia tumbo lake ikiashiria kuwa anapata maumivu makali ya tumbo.

Maumivu ya Tumbo chini ya Kitovu kwa Wanawake, Sababu na Tiba

Maumivu ya tumbo huwakuta wanawake wengi kwenye umri tofauti tofauti katika maisha yao.

Kuna sababu mbalimbali za maumivu ya tumbo kwa wanawake.

Kwenye makala hii tufahamu sababu mbalimbali zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo hasa chini ya kitovu kwa wanawake.

Hizi ni sababu za mara kwa mara zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa wanawake.

Maumivu ya hedhi.

Maumivu ya hedhi ni moja ya maumivu ya mara kwa mara kwa wanawake, maumivu ya hedhi yanaweza kuwa kabla, baada au wakati wa hedhi.

Maumivu ya hedhi huwa chini ya kitovu ila muda mwingine yanaweza kusambaa mpaka chini ya mgongo.

Mimba:

Mimba pia ni sababu ambayo inaweza kusababisha maumiu chini ya kitovu kwa wanwake.

Maumivu ya tumbo huja kwasababu ya mabadiliko mbalimbali yanayotokea kwenye viungo vya uzazi wakati wa ujauzito kujiandaa kutunza mtoto.

Mimba kutunga nje ya kizazi:

Moja ya dalili ya mimba iliyotunga nje ya kizazi ni kupata maumivu makali ya ya tumbo hasa maumivu ya tumbo chini ya kitovu.

Mkojo mchafu (UTI):

Maambukizi kwenye njia ya mkojo au mkojo mchafu ni moja ya sababu ya maumivu ya tumbo kwa wanawake hasa chini ya kitovu.

Maumivu ya mkojo mchafu huambatana na dalili nyingine kama vile maumivu wakati wa kukojoa au kuhisi kukojoa mara kwa mara hata kama mkojo hakuna.

Maambukizi ya magonjwa kwenye viungo ya uzazi:

Kama mwanamke amepata maambukizi kwenye viungo vyake vya uzazi kunaweza kumsababishia mauivu ya tumbo chini ya kitovu.

Mara nyingi maambukizi hayo husababishwa na magonjwa ya zinaa kwa wanawake.

Maambukizi ya magonjwa ya zinaa kwa mwanamke yanaweza kuambatana na dalili kama vile maumivu wakati wa tendo la ndoa, kutoka vitone vya damu au kutokwa na uchafu ukeni unaotoa harufu mbaya.

Tumbo kujaa gesi:

Tubo kujaa gesi ni sababu nyingine inayoweza kusababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa wanawake.

Gesi tumboni inaweza kusababishwa na kumeza hewa au matokeo ya vijidudu kwenye utumbo kumengenya chakula na kuzalisha gesi kwenye utumbo.

Ni hali ya kawaida kuwa na gesi kwenye utumbo ila inapozidi inaweza kuwa ni dalili ya tatizo kwenye mfumo wa chakula.

Kidole tumbo:

Kidole tumbo ni kisehemu kidogo kwenye makutano ya utumbo mpana na utumbo mwembamba.

Kuna muda kidole tumbo kinaweza kuathirika kusababisha kuvimba.

Tatizo la kidole tumbo husababisha maumiu ya tumbo ya tumbo chini ya kitovu.

Zingatia:
Maumivu ya tumbo chini ya kitovu yanapozidi kuwa makali zaidi au ya muda mrefu ni vizuri kumuona daktari kwa msaada zaidi.

1
1
1