Muonekano wa Giza:

Msaada

Picha inamuonesha mwanamke akiwa amekaa kitandani akionekana ni mwenye mawazo mengi akiwa ameshika kichwa na 
	nyuma yake kuna mwanaume akiwa amejilaza kitandani.

Maumivu wakati wa Tendo la Ndoa kwa Wanawake

Wanawake wengi wanaweza kupitia changamoto ya kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa katika kipindi flani kwenye maisha yao.

Wanaweza kupata maumivu kabla ya tendo la ndoa, wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo la ndoa.

Tuzifahamu sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa kwa wanawake.

Kutokuwa na uteute wa kutosha ukeni:

Moja ya sababu ni kutokuwa na uteute wa kutosha ukeni, hali hii inaweza kusababishwa na kushuka kwa kiwango cha homoni ya Estrogen kwa mwanamke.

Kushuka kwa homoni ya Estrogn kunaweza kusababishwa na mwanamke kufikia ukomo wa hedhi, kama ametoka kujifungua au akiwa ananyonyesha.

Pia kuna baadhi ya madawa mwanamke akiyatumia yanaweza kusababisha kupungua kwa uteute ukeni.

Majeraha ukeni.

Sababu nyingine ni majeraha ukeni ambayo yanaweza kuwa yametokana na ajali au alifanyiwa upasuaji kwenye viungo vya uzazi.

Pia kama mwanamke alishawahi kufanyiwa ukeketaji au alichanwa ili kuongeza njia wakati wa kujifungua.

Yote yanaweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke.

Magonjwa ukeni au magonjwa ya ngozi.

Magonjwa ukeni au magonjwa kwenye njia ya mkojo pia yanaweza kusababisha maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa kwa wanawake.

Pia kuna sababu za kisaikolojia ambazo zinaweza kusabaisha maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa kwa mwanamke.

Sababu hizo ni kama vile msongo wa mawazo, wasiwasi, uwoga na matatizo ya kimahusiano yanaweza kusababisha mwanamke kutokuwa na msisimuko wakati tendo na kumsababishia maumivu

Pia baadhi ya wanawake ambao wameshawahi kufanyiwa unyanyasaji wa kingono wanaweza kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Mara nyingi maumivu haya huwa ni ya muda mchache.
Kama utaona maumivu wakati wa tendo yanaendelea kwa muda mrefu ni vizuri kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.

0
0
1