Sababu kuu ya wanaume kulala baada ya tendo la Ndoa
Kuna sababu mbalimbali zinazosababisha wanaume kulala baada ya kufanya tendo la ndoa.
Kuna sababu za kimazingira na za kisaikolojia ambazo zinaweza kusababisha mwanaume kulala mara baada ya kufanya tendo la ndoa.
Ila sababu kuu ni ya kibaiolojia na jinsi ubongo wa wanaume unavyofanya kazi.
Kwa mujibu wa mtandao wa kisayansi wa live science.
Tafiti za kisayansi zimeonesha kuwa ubongo wa mwanaume hutoa kemikali na homoni nyingi baada ya mwanaume kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa.
Moja kati ya homoni zinazotolewa kwa wingi baada ya mwanaume kifika kileleni ni homoni inayoitwa prolactin.
Homoni ya prolactin utolewa kwaajili ya kumridhisha mwanaume anapofika kileleni na kuuanda mwili wa mwanaume kwaajili ya kurudia tena tendo.
Na tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa wanaume wenye upungufu wa homoni hii hutumia muda mfupi kupumzika na kurudia tena tendo kwa mara nyingine.
Pia kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisayansi homoni hiyo hupatikana kwa wingi wakati wa usingizi.
Homoni hiyo ilijaribiwa kwa kuwekwa kwa wanyama na baada ya muda mchache wanyama hao walionekana kuchoka.
Kwasababu hiyo homoni hiyo inayotolewa kwa wanaume wanapofika kileleni inaweza kuwa na mahusiano makubwa na sababu ya wanaume kulala baada ya tendo la ndoa.
Pia kuna baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa homoni hiyo hutolewa mara 4 zaidi kwa wingi kwa wanaume wanaofanya tendo la ndoa kuliko kuliko kwa wanaume wanaojichua.
Oxytocin na vasopressin ni homoni nyingine ambazo hutolewa kwa wingi mwanaume anapofika kileleni.
Homoni hizo pia zinahusishwa na sababu ya mwanaume kulala mara baada ya tendo la ndoa.
Homoni ya oxytocin inadhaniwa kusaidia kupunguza msongo wa mawazo kwa mwanaume, hali hiyo nayo inaweza kuchangia kwa mwanaume kulala mara baada ya kufanya tendo la ndoa.
Unaweza pia kusoma: