Muonekano wa Giza:

Msaada

Picha inaonesha kielelezo cha mtu ambaye ameshikilia sehemu ya kushoto ya kifua chake kuonesha kuwa anapata maumivu makali kwenye kifua, picha imeambatanishwa
	na kielelezo cha moyo wa binadamu na mishipa ya damu iliyojaa mafuta kwenye kuta zake.

Shinikizo la Juu la Damu (Presha ya Kupanda) Mambo hatarishi na Jinsi ya kujilinda

Tatizo la Shinikizo la damu au presha ni hitilafu ndani ya mwili inayosababisha mapungufu kwenye mishipa ya damu, mapungufu hayo yanaweza kusababisha presha ya damu kupanda au kushuka.

Kwa presha ya kupanda ili damu ipite kwenye mishipa inahitajika nguvu kubwa ya kusukuma damu hivyo moyo unatumia nguvu kubwa kusukuma damu mwilini.

Kipimo cha shinikizo la damu kinapimwa kwa milimita za zebaki au mercury.

Kipimo hicho kinapozidi milimita 130 kwa 80 mtu huyo anahesabika kuwa ana shinikizo la juu la damu au presha ya kupanda.

Ikiwa tatizo la shinikizo la damu halitatibiwa mapema inaongeza hatari ya mtu kupata shambulio la moyo, kiharushi na matatizo mengine makubwa mwilini.

Inashauriwa kuwa na utaratibu angalau kila baada ya miaka 2 kupima presha yako unapofikisha umri wa miaka 18 na kuendelea.

Mtindo mzuri wa maisha kama vile kuacha uvutaji wa sigara, kufanya mazoezi na kula vizuri ni kinga bora na tiba nzuri ya tatizo la shinikizo la damu japo si kwa wote kuna baadhi ya watu inawalazimu kutumia damu kutibu tatizo hilo.

Asilimia kubwa ya watu wanaishi na tatizo la shinikizo la damu bila kujua wala kuhisi chochote.

Unaweza kuwa na tatizo la shinikizo la damu kwa miaka bila kuona dalili zozote.

Kuna baadhi ya watu hupata dalili kama vile:

Na mara nyingi dalili hizi huonekana kwenye hatua ambayo tatizo la shinikizo la damu limefikia hatua ya kuhatarisha afya yako.

Kuna sababu kadhaa ambazo zinaweza kusababisha tatizo la shinikizo la damu:

Kuganda kwa mafuta mabaya ya cholesterol kwenye mishipa ya damu:

Hali hiyo husababisha damu kushindwa kupita vizuri na kuufanya mayo kutumia presha kubwa kusukuma damu.

Pia Kuna baadhi ya matatizo ndani ya mwili mtu akiwa nayo yanaweza kusababisha tatizo la shinikizo la damu.

Na kuna baadhi ya madawa yanaweza kusababisha tatizo la shinikizo la damu.

Mbali na sababu hizo pia kuna baadhi ya mambo ambayo humuongezea mtu hatari ya kupata tatizo la shinikizo la damu.

Kuwa na umri mkubwa, kwa wanaume wenye zaidi ya miaka 64 na wanawake wenye umri zaidi ya miaka 65 wapo kwenye hatari kubwa zaidi.

Kama kwenye familia yako kuna historia ya wazazi au ndugu zako wa karibu wenye tatizo la presha upo kwenye hatari ya kupata tatizo hilo.

Kuwa kibonge au kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi kunasababisha mabadiliko mengi kwenye viungo ndani ya mwili, mabadiliko hayo yanaweza kusababisha kuongezeka kwa shinikizo la damu mwilini.

Tabia bwete au kutokuwa na tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara inaongeza hatari ya mtu kupata tatizo la shinikozo la dammu.

Uvutaji wa sigara au matumizi mengine ya tumbaku kunaweza kuathiri mishipa ya damu na kusababisha tatizo la shinikizo la damu.

Matumizi ya chumvi kwa wingi yanasababisha kuongezeka kwa madini chumvi ya sodium mwilini yanayopelekea kuongezeka kwa ujazo wa damu na kuongezeka kwa shinikizo la damu.

Unywaji wa pombe kupita kiasi umeonekana kuongeza hatari zaidi ya tatizo la shinikizo la damu hasa kwa wanaume.

Kuwa na msongo wa mawazo nako kunaongeza hatari ya tatizo la shinikizo la damu.

Pia kwa mwanamke mjamzito moja kati ya mabadiliko anayoyapata kipindi cha ujauzito ni kuongezeka kwa shinikizo la damu.

Pindi unapogundulika kuwa na tatizo la shinikizo la damu ni muhimu kuchukua hatua na kufuata ushauri wa wataalamu kudhibiti kiwango cha presha.

Kuchelewa kudhibiti kiwango cha presha kunaweza kusababisha matatizo mengine makubwa mwilini:

0
0
1