Muonekano wa Giza:

Msaada

Picha inamuonesha mwanamke akiwa amejilaza kwenye kochi huku akiwa ameshikilia tumbo lake na kukunja sura yake kama ishara ya kuwa 
	anapata maumivu makali ya tumbo.

Sababu za kukosa Hedhi kwa Mwanamke baada ya Kuvunja Ungo

Kwa kawaida mwanamke wote wenye wastani wa umri kati ya miaka 12 mpaka 49 hupata hedhi kila mwezi.

Mzunguko mzima wa hedhi kwa mwanamke kawaida ni wasatani wa siku 28 mpaka 30.

Mzunguko wa hedhi kwa mwanamke lengo ni kumuandaa mwanamke kwaajili ya kubeba mimba.

Inapotokea mwanamke ajapata mimba kwa mwezi huo kuta za mfuko wa kizazi zilizoandaliwa kwaajili ya kupokea mimba hutolewa nje kama damu ya hedhi.

Katika makala hii tuangalie sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha mwanamke kukosa hedhi kwa zaidi ya miezi 3 au zaidi.

Linapokuja swala la mwanamke kukosa hedhi inachukuliwa kama ni tatizo ikiwa kama mwanamke hajaona siku zake kwa miezi mitatu au zaidi na wanamke sio mjamzito wala sio mwanamke anayenyonyesha.
Pia kama ni mwanamke wenye umri kati ya miaka 15 mpaka 50.

Tatizo la kukosa hedhi kwa wanawake lipo kwa aina mbili tofauti, kuna Primary na Secondary.

Ikiwa binti wa kike hajaona hedhi na amefikia au amepita umri wa kawaida wa mwanamke kuvunja ungo ambao unakadiriwa miaka 15 hali hiyo huitwa primary.

Pia kwa mwanamke ambaye alikuwa anapata hedhi kawaida na ghafla akawa hapati tena hedhi hali hiyo huitwa secondary.

Kuna baadhi ya dalili ambazo zinaambatana na tatizo la kukosa hedhi kwa mwanake, dalili kama vile;

Hizo zote ni dalili ambazo mwanamke mwenye tatizo la kukosa hedhi anaweza pia kuziona.

Kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha mwanamke kukosa hedhi.

Kwa mabinti wa kuvunja ungo ila hawakuwahi kupata hedhi sababu zinazoweza kusababisha hali hiyo ni kama vile:

Kwa wanawake ambao walikuwa kwenye hedhi kawaida, tatizo la kukosa hedhi husababishwa na sababu kama vile:

Sababu zingine zinazoweza kusababisha hali hii ni kama vile, msongo wa mawazo, lishe duni, mabadiliko ya uzito kama vile kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi au kuwa na uzito mdogo kupita kiasi.

Kufanya mazoezi makali kuliko kawaida na kuna baadi ya dawa ambazo mwanamke akizitumia zinaweza kusababisha kukosa hedhi.

Na pia kuna baadhi ya magonjwa kwa mwanamke yanaweza kusababisha tatizo la kukosa hedhi kama vile magonjwa ya figo.

Unapaswa kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi ikiwa ni binti na umefikia umri wa kuvunja ungo na hujawahi kupata hedhi au kama imepita miaka 5 hujapata hedhi tokea umeona dalili za kupevuka kama vile kuota matiti.

Vile vile inapaswa kumuona daktari kama umepitiliza miezi mitatu au zaidi bila kuona hedhi.

1
0
1