Yafahamu Mambo haya muhimu kuhusu Uvimbe kwenye Kizazi kwa Mwanamke
Inakadiriwa kati ya asilimia 20 mpaka 80 ya wanawake wanaweza kuwa wamepata uvimbe kwenye kizazi mpaka kufikia miaka 50.
Asilimia 99 ya uvimbe kwenye kizazi haisababishi madhara makubwa ya kiafya.
Kuna baadhi ya vimbe kwenye kizazi zinaweza zisionekane na baadae hupotea zenyewe bila matibabu yoyote pia kuna baadhi ni kubwa kiasi cha kuweza kuguusa kwa kupapasa tumbo.
Uvimbe unaweza kuwa mmoja au vimbe zaidi ya moja sehemu tofauti tofauti kwenye kizazi.
Dalili za uvimmbe kwenye kizazi hutofautiana kulingana na ukubwa wa uvimbe, mahali ulipo na idadi ya uvimbe kwenye kizazi.
Kuna baadhi ya watu hawaoneshi dalili zozote pia kuna wengine hupata dalili kama vile:
- Kuwa na hedhi ya muda mrefu zaidi ya wiki moja.
- Kuwa na damu nzito ya hedhi.
- Kutokwa na vitone vya damu au kubleed katikati ya mzunguko wa hedhi.
- Maumivu ya kiuno na mgongo.
- Kukojoa mara kwa mara.
- Kupata shida ya wakati wa kutoa mkojo.
- Kupata choo kigumu na kupata shida ya kushika ujauzito.
Hizo ni dalili za mtu ambaye ana uvimbe kwenye kizazi kwa kutegemea ukubwa wa uvimbe, mahali uvimbe ulipo na idadi ya vimbe kwenye kizazi.
Hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kusababisha uvimbe kwenye kizazi kwa wanawake ila kuna sababu mbalimbali ambazo zinamuweka mwanamke katika hatari ya kupata uvimbe kwenye kizazi kama vile:
Umri:
Hasa kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 30 mpaka 50 wapo kwenye hatari zaidi ya kupata uvimbe kwenye kizazi.
Uzito mkubwa:
Sababu za kuzaliwa nazo, hasa kama kwenye familia kuna mtu amewahi kupata uvimbe kwenye kizazi kuna uwezekano wa kurithisha vizazi vinavyofuata.
Sababu zingine ni kama mwanamke amewahi kuvunja ungo mapema kabla ya kutimiza miaka 10.
Na kwa wanaweke wenye shinikizo la damu wako kwenye hatari zaidi ya kupata uvimbe kwenye kizazi.
Kuna baadhi ya mambo ambayo yanashauriwa kufanya yanaweza kusaidia kukukinga usipate uvimbe kwenye kizazi na kama una uvimbe inaweza kusaidia kupunguza uvimbe.
Kwa mujibu wa tafiti uliofanywa waka 2018 inashauriwa,
- Kufanya mazoezi mara kwa mara.
- Kuzingatia mlo kamili.
- Kupunguza msongo wa mawazo.
- Kuachana na uvutaji wa sigara, unywaji wa vinywaji vyenye caffeine kama vile kahawa au energy drink, na kuachana na unywaji wa pombe.
Utafiti wa hivi karibuni umeonesha kuwa upungufu wa vitamin D mwilini unaongeza hatari ya kupata uvimbe au kuongeza ukubwa wa tatizo.
Hivyo ni muhimu kuzingatia ulaji wa vyakula vyenye vitamin D kwa wingi.
Pia kama mtu anasumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu anashauriwa kufanya mambo yafuatayo ili kudhibiti shinikizo la damu.
- Kupunguza ulaji wa nyama nyekundu, chumvi na sukari kwa wingi.
- Kuwa na tabia ya kupima mara kwa mara kuangalia kiwango wa presha uliyonayo.
- Kuwa na tabia ya kwenda kufanya check up mara kwa mara.
- Kuzingatia ushauri wa daktari na dawa kwaajili ya kurekebisha shinikizo la damu.
- Na kuzingatia kufanya mazoezi mara kwa mara.
Uvimbe kwenye kizazi kwa kawaida hukua taratibu sana na wakati mwingine hukaa tu bila kuongezeka ukubwa.
Mara nyingi uvimbe kwenye kizazi unapotea wenyewe hasa mara baada ya mwanamke kufikia ukomo wa hedhi.
Hivyo unaweza usihitaji matibabu isipokuwa tu kama unasumbuliwa na dalili za uvimbe kwenye kizazi na unakupa changamoto za kiafya ni muhimu kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.
Unaweza pia kusoma: