High School - Episode 01 
Jina langu ninaitwa Catherine Kindamba.
Ilikua ni siku ya Jumanne nilipowasili shuleni Hans pope Academy mkoani Mwanza kutoka Dar es salaam.
Nilimaliza kidato cha nne katika shule ya secondary Canossa na kupata division one na kisha kuchaguliwa
kujiunga katika shule ya secondary Kibasila kwa mchepuo wa ECA, yani Economics, commerce na Accountancy.
Baba yangu hakuyapenda kabisa mazingira ya pale Kibasila, hivyo aliamua kuniamishia Hans pope Academy Mwanza.
Ni kiasi kama mwenzi wa pili niliamia shuleni hapo. Mimi ni msichana mpole na mwenye ushirikiano na wenzangu.
Ninapenda dini na kulelewa kimaadili. Marafiki wawili tu Winnie na Angel walitosha kuifanya jamii yangu ndogo.
Daima sikupenda company ya wavulana kwakuwa sikupenda vile baba alivyokuwa akimfanyia mama, hali iliyopelekea kuwepo
kwa migogoro isiyoisha pale nyumbani.
Pamoja na hayo yote baba yangu ambaye alikuwa mhasibu wa pale bandarini pamoja na mama yangu ambaye alikuwa
mwalimu wa shule ya msingi ya Academy International school niliyosoma hapo awali walinipenda sana nikiwa kama
mzaliwa wa pekee.
Mazingira ya shule mpya ya Hans pope Academy yalikuwa mazuri niliyapenda.
Ilifika jioni saa moja nikaingia chumba nilichopangiwa katika jengo lililoitwa white house nikalala fofofo.
Saa kumi na mbili kamili ya alfajiri nilishtushwa na mlio wa kengele, nilishuka dekani kwangu na hapo ndipo
niligundua kuwa sikuwa peke yangu. Kilikuwa ni chumba kidogo kizuri kilichopangiliwa vizuri, cha watu wawili.
Kulikuwa na makabati mawili makubwa yaliyojigawa ukutani, meza ya kusomea na madirisha mapana ambayo yaliweza
kuingiza mwanga na hewa safi.
Katika kitanda cha chini alikuwepo msichana ambaye pamoja na kuwa alikuwa bado usingizini haikuniwia vigumu
kujuwa kuwa huyu kiumbe aliyeko mbele yangu ni mzuri na mrembo wa kutosha kutwaa taji la miss Dunia.
Ninajiamini kuwa mimi ni mzuri huyu msichana hakika alikuwa shani mbele ya macho yangu.
Nilimsanifu kuanzia sura yake zuri, lips zake ambazo kwa juu zilichora kama umbo la kopa, rangi yake nyeupe ya kung’aa,
ngozi yake laini, shape yake, hakika huyu msichana alikuwa ni mzuri sana.
Nilimuangalia hadi macho yangu yalipotosheka kisha nikasimama tu nisijue nini cha kufanya nikageuka kwenda sehemu
ambayo niliweka mabegi yangu.
“Wewe ni nani.”
Sauti tamu ilipenya katika masikio yangu.
Niligeuka kwa mshituko na kutazama pale sauti ilipotokea.
Yule mrembo wa dunia alikuwa bado amelaa alikuwa akiniangalia macho yake makubwa na matamu yalitosha kunihakikishia
kuwa huyu msichana aliumbwa kwa utulivu zaidi.
“Aaaaah aaaaa mimii.”
Nilishikwa na kigugumizi sikujua nimjibu nini kile kitu kilinichanganya.
“Naitwa Catherine Catherine Kindamba”
Hatimaye niliweza kuongea na kujitambulisha.
“Catherine unafanya nini hapa.”
Aliongea huku akinyanyuka kutoka kitandani.
“Mimi ni mgeni nimefika hapa jana usiku, nimehamia.”
Niliongea.
“Mmmh.”
Alinitazama kwa Dharau huku akibetua midomo yake.
“Catherine karibu.”
“Ahsante.”
Nilijibu.
“Sasa umeamka saizi unaenda wapi.”
Aliniuliza.
“Aaaaah nimesikia kengele nataka nijue ni nini kinaendelea.”
“Oooh sasa hivi ni muda wa jogging kama unapenda nenda ila sio lazima sana unaweza kubaki hapo ukijiandaa kwa ajili
ya kuingia darasani, mi pia nipo siendi jogging.”
“Aaaaah sawa hata mimi pia sipendelei jogging acha nipange vitu vyangu.”
Niliongea.
“Ooooh unasoma Combination gani?”
Aliniuliza.
“Niko ECA.”
Nilijibu.
“Ooooh.”
“Wewe je unaitwa nani.”
Nilimuuliza.
“Naitwa Candy, niko HGE na ukipenda unaweza kuniita Queen Candy.”
Alisema.
Hakika nilijua kwamba huyu msichana aliyekuwa mbele yangu ni mtu mwenye dharau sana hata hivyo sikuwa na papara
dharau zake hazikuwa kitu kwangu lakini katika siku hizo za mwanzo ilikuwa ni hali ya kawaida tu kwakuwa nilihitaji
kuijua shule vizuri sikumtilia maanani sana.
Nilifanikiwa kupanga vitu vyangu katika mpangilio uliopendeza mbele za macho yangu baada ya hapo nilijiandaa kwa ajili
ya ratiba za siku hiyo.
Uniform mpya zilinipendeza hakika, sketi yangu fupi nyeusi iliyochanua vyema, shati langu jeupe la mikono mirefu,
tai ya pundamilia, soksi ndefu zilizonifika magotini na viatu nilipendeza sana.
Muda ulipokaribia mimi na Candy tuliongozana hadi mstarini na baada ya matangazo machache tuliruhusiwa kuingia madarasani.
Candy aliniongoza mpaka kwenye darasa letu.
Ili ndilo darasa lako aliongea kwa dharau na kisha akaondoka kwa hatua za mikogo, nilibaki nikimtazama mpaka alipopotelea.
Hakika Candy ni msichana mzuri niliwaza.
Dakika moja ya kumshangaa Candy ilipoisha niliamua kuingia darasani na wakati huo naingia darasani nilijigonga kwenye
paji la uso mlangoni.
Nilihisi maumivu makali.
Madaftari mawili ambayo hayakutosha kwenye kibegi changu cha mgongoni yalidondoka.
Nilichutama ili kuyaokota na hapo nilijigonga tena na safari hii sio kwenye mlango tena bali ni mtu alikuwa amenigonga,
nilikasirika sana.
Nikageuka kwa ghadhabu ili nimuone ni nani ambaye amenigonga nilikutana na sura nzuri ya kiume
iliyopambwa na tabasamu laini, hakika sikuwahi kukutana nalo katika maisha yangu yaliyopita.
“Sorry.”
Alisema kwa sauti tamu.
“Aaaanh usijali nilikua nakusaidia kuokota madaftari yako lakini kwa bahati mbaya nikakugonga samahani kwa hilo.”
“Usijali na asante sana.”
Nilisema.
Aliniokotea madaftari yangu na kisha akanikabidhi.
“Wewe ni mgeni mahali hapa sijawahi kukuona.”
“Ndio nimehamia jana.”
“Karibu sana.”
“Asante.”
Nilisema.
“Unasoma combination gani?”
“Niko ECA.”
“Wooow karibu kwenye darasa letu.”
“Asante.”
“Naitwa Martin, sijui wewe unaitwa nani?”
“Naitwa Catherine.”
“Catherine karibu sana.”
“Asante.”
Alinishika mkono na kuniongoza darasani, alisimama mbele ya darasa na kuongea kwa sauti nzuri ya kiume.
“Hello class huyu ni mwanafunzi mpya atajitambulisha anahitaji ushirikiano wenu.”
Akaniachia nafasi nijitambulishe mbele ya darasa.
Nikasema kwa uwoga hali nimeshikwa na aibu za kike.
“Hello class naitwa Catherine nimetokea Kibasila.”
Nilishindwa kuendelea, watu walicheka na kisha wakanikaribisha.
Nilioneshwa sehemu ya kukaa pembeni yangu aliketi msichana mzuri alinisalimia.
“Hello naitwa Martha karibu sana.”
Nilitabasamu na kisha nikamwambia asante.
Ghafla mwalimu aliingia akiwa mwenye ghadhabu, tulisimama kumsalimia. Hakujibu salamu yetu alianza kufoka.
“Kama hujafanya assignment simama hivyohivyo na kama umefanya kaa chini.”
Nilijikuta nimesimama peke yangu.
“All eyes on me.”
Nilihisi nimejisemea mwenyewe lakini kumbe niliongea kwa sauti darasa zima wakacheka, nikatoa macho hali nimeachia mdomo.
Mwalimu aliniuliza.
“Je wewe ndio ambaye ujafanya kazi yangu ni kitu gani kimekufanya usifanye assignment?”
Nilishikwa na kigugumizi.
“Eeeeh aaanh mimi ni mgeni.”
“Ahaaa.”
Alisema mwalimu yule ambaye baadae nilikuja kumtambua kama Mr. Maloya.
“Kaa chini.”
Nikakaa.
Alianza kufundisha huku akitumia muda wake mwingi kunitazama, sikujua kwa sababu ya ugeni wangu au vipi.
Tuliendelea na vipindi mpaka wakati wa mapumziko ulipofika. Darasa zima waliondoka.
Nilibaki peke yangu nisijue wapi pa kuelekea. Na wakati nimeinama nikifuta viatu vyangu nilisikia nimeguswa begani kwangu.
Kwa kuwa sikuwa nimemzoea mtu yeyote nilijua lazima ni Candy ambaye amenipitia kwa ajili ya mapumziko.
“Candy.”
Niliita huku nikigeuka, hakuwa Candy nilikutana na sura nzuri ya kiume.
“Martin hapa.”
Niliachia tabasamu.
“Oooh Martin.”
Nilishindwa kuendelea.
“Mbona uko hapa peke yako?”
Aliuliza.
“Sijui nielekee wapi.”
Nikasema.
“Aaanh ngoja twende restaurant.”
Nikanyanyuka tukaongozana.
Tulipofika niliagiza maziwa na slace tatu za mkate.
“Unayaonaje mazingira ya shule yetu.”
Aliuliza.
Kabla sijamjibu msichana ambaye alikuwa mmoja kati ya wanafunzi alifika mezani kwetu.
“Wewe ndio Catherine si ndio?”
Aliuliza.
“Ndio.”
Nilimjibu.
“Academic master kasema upeleke barua zako za uhamisho ofisin kwake sasa hivi.”
Alisema.
“Asante kwa taarifa.”
Nilijibu.
Nilinyanyuka haraka bila kuaga na kuelekea yalipo mabweni yetu.
Nilipofungua nilishangaa kumkuta Candy amelala usingizi, nikashangaa wakati wa mapumziko Candy amelala kwa uchovu gani.
Sikumtilia sana maanani kwa vile nilikuwa mgeni, nikachukua barua zangu na kuzipeleka panapohusika na kisha kurejea darasani.
Masomo ya siku hiyo yaliendelea kama kawaida.
Muda wa vipindi ulipoisha nilirejea bwenini na wakati huo Candy ndio alikuwa akiamka, tulipata chakula cha mchana na kisha kwenda kwenye michezo.
Wakati wa jioni ulipofika tuliingia kwenye kusali. Nilikaribishwa vizuri sana nilijihisi ni mmoja kati yao.
Nilipata faraja mno kwa vile nilikuwa nikikubalika kila sehemu.
Maisha ya shule yaliendelea vizuri.
Niliyazoea mazingira ya shule mpya, ilikuwa ni shule ya kifahari ambayo haikuwa rahisi kwa mtu wa kawaida kuweza kumsomesha mtoto wake.
Ufaulu wangu pia ulikuwa juu.
Mwalimu Maloya ambaye alikuwa ni mwalimu wa mazingira alikuwa akifatilia maendeleo yangu kwa ukaribu zaidi,
mara zote nilipokosea aliniita ofisini kwake na kunionya.
Na wakati nilipofanya vizuri hakusita kunisifia mbele ya watu, nilimpenda kwakuwa alijali maendeleo yangu.
Candy aliendelea na tabia yake ya kulala kila mara, mara nyingi nilimkuta amelala wakati wa vipindi, nilijua ndio aina yake ya maisha
aliyokuwa akiishi tangu alipofika shuleni kwani pamoja na tabia yake ya kulala kupitiliza Candy alikuwa vizuri kimasomo,
kitaaluma alikuwa juu na alikuwa akiwaongoza wenzie darasani.
Dharau za Candy zilizidi maradufu sikujali kabisa.
Urafiki wangu na Martin ulizidi kadri siku zilivyozidi kwenda, alikuwa ni mvulana mwenye kujali, mpole na mwenye haiba nzuri.
Mwanzoni sikupenda kampani ya wavulana, lakini kutokana na haiba yake niliweza kumzoea na tulishirikiana kwenye masomo na
kuweka ushindani baina yetu.
Nilikuja kugundua martin ni raisi (kiranja mkuu wa shule) na pia alikuwa ni kiongozi wa kwaya kwenye jumuiya yetu kanisani.
Alipenda kuimba na alikuwa na sauti nzuri sana.
Pia nilikuja kujua kuwa Candy alikuwa ni kiongozi wa mazingira.
Candy alianza tabia ya kujiandaa alfajiri mapema kabla sijaamka kila nilipoamka nilikuta tayari ameshamaliza na wakati mwingine
alishaondoka.
Hakuwa na nafasi katika akili yangu hivyo nilimpotezea.
Unaweza pia kusoma: