Wakati Nilipokufa - Episode 04 
“Hivi wewe unataka nini? Unataka utuue na sisi kabisa.”
Nilitegemea shangazi angemtetea mke wangu lakini ndiyo kwanza alianza kumsema.
“Mnamkosea sana huyu binti.”
Aliongea mama yangu mkubwa huku nikisimama tu mlangoni nikiwa ninawasikiliza.
Na kwa bahati nzuri kwenye lile geti niliweza kuwaona bila wao kuweza kuniona.
Mke wangu alisimama pale huku amemshikilia mtoto wetu Hasan na mabegi yake yakiwa pembeni huku ameinama
machozi yakimtiririka.
Mama yangu mkubwa alisimama na kisha kuongea.
“Huyu binti hana makosa yoyote na ana mtoto mnapomfukuza aende wapi?
Stori yake yote mnaijua mbona mnamfanyia hivyo mwenzenu.”
“Inamaanisha wewe hujui kama huyu alibeba mimba ya kaka yetu ili tu achukue mali zake.
Huyu mtoto ni yatima kaka yangu alikutana nae tu akamtegeshea mimba ili azae nae.”
“Hata kama.”
Mama mkubwa aliongea.
“Pamoja na hayo Mudi mwenyewe alimkubali na akawa anaishi nae kama mkewe miaka sita amemtunza, leo kwanini
mnamfukuza na ana watoto aende wapi?”
Aliongea mama mkubwa.
Watu wote walicheka mule ndani.
“Sasa sikiliza, wewe kama unataka kumsaidia mchukue uende nae kwako. Wewe Aisha ondoka hapa ndani, uwifi sijui
kama tulikuwa tuna undugu wowote, mahusiano yoyote yameishia hapa tunaomba uondoke. Na usitake ukaniletea ugomvi nisije
nikakuitia polisi wakutoe hapa kwa nguvu ondoka mwenyewe nilishakufukuza nashangaa umerudi tena, sitaki kuona sura yako hapa.
Muone ulivyo na sura mbovu.”
Aliongea dada yangu.
Wala hata akusubiri ajibiwe aliendelea kumwaga chenji aliongea maneno machafu sana.
“Toa uso wako mchafu hapa nisije kutapika mimi.”
Nilishindwa kuvumilia nilifungua geti na kuingia kwa nguvu.
Kila mtu aliyeniona mule ndani alipiga kelele.
“Mama nakufaaa…”
Watu walihisi wameona jini hata hivyo mimi ndiye niliyekuwa nimesimama mlangoni iliwawia vigumu sana kutoka kwasababu
mara nyingi mlango wa nyuma tulikuwa tukiufunga.
Kila mtu alikimbilia kwenye pembe yake huku akiziba sura asinione.
“Inatosha sasa Salma.”
Niliongea kwa sauti ya kilio.
“Siamini kama leo hii nyie ni ndugu zangu, kwahiyo mara baada ya kuambiwa mimi nimekufa ndiyo mkaamua kuifanyia hivi
familia yangu? Salma hata wewe!”
Niliongea.
Salma alishindwa kuamini.
“Mudi hujafa?”
Aliniuliza.
“Kwahiyo ulitaka nife ili uinyanyase familia yangu? Sasa kitu gani ambacho kinawafanya muwafukuze? Kama ni yale maduka si
ungebaki nayo tu ungewaacha watoto wangu waendelee kujibangaiza na mama yao hapa ndani umewafukuza waende wakaishi wapi?”
Niliongea kwa sauti ya machozi.
Chozi la aibu lilimdondoka Salma.
Hata ndugu zangu wengine waliona aibu sana.
Kiukweli nimeshindwa kuelewa kabisa.
“Salma…”
Nilimuita.
Aliporomoka mpaka chini mpaka akipiga magoti.
Aliniinamia.
“Kaka ni shetani tu.”
“Sawa.”
Nilijibu.
Alinyanyua uso wake kwa gafla na kuniangalia.
“Ni shetani naelewa, sasa naomba wewe na kikundi chako chote muondoke mkafuatane na huyo shetani. Mama mkubwa naomba ubaki hapa.”
Nilisema.
Mama mkubwa alionekana kutokuamini.
“Nyie wengine wote undugu wetu umeishia hapa naombeni mtoke.”
Niliwafukuza kwa nguvu.
“Toka Salma sitaki kukuona.”
Hakuamini kilichokuwa kikiendelea.
Sikutaka tena kuwa na undugu nae.
“Mume wangu…”
Aliniita mke wangu.
“Nyamaza kimya.”
Nilifoka.
Na yeye alitii.
Niliwakukusa watu wote waliokuwepo mule ndani niliwafukuza na kuwasukumiza nje.
Sikujali kama walianguka, waliumia, sikujali kabisa.
Mara baada ya kuwatoa watu wote mule ndani nilipiga magoti na kisha kuanza kumuomba msamaha mke wangu mbele ya mama yangu mkubwa.
Nilimuelezea kila kitu kuhusiana na vyote ambavyo nilikuwa nikifanya kwa machozi.
Nilimuelezea juu ya mali zangu zote nilizoachiwa.
Mke wangu alilia sana.
“Ulikosea sana.”
Alisema mama mkubwa.
“Unapooa unamaanisha kwamba unaacha familia yako unaambatana na mkeo.”
Aliongea mama yangu mkubwa ambaye alikuwa ni mkristo.
“Inamaanisha uiache kabisa familia yako ukaanze familia mpya na mkeo lakini wewe ulichukua tu mwanamke ukawa
unaishi naye bila kutambua thamani yake bado mambo yako mengi unaishirikisha familia yako, ukae ukijua kwamba mkeo ni
ndugu yako wa kwanza ulitakiwa umuheshimu mkeo na kumpenda. Sisemi kwamba uachane na familia yako uwatelekeze kabisa hapana
lakini mke wako alitakiwa kuwa ni mtu wako wa kwanza kwasababu huyu ni mwili mmoja na wewe. Kigezo cha kwanza hamkufunga ndoa
kisiwe sababu ya kuwafanya ushindwe kumshirikisha mkeo katika mambo yako.”
Mke wangu aliendelea kulia tu.
Maneno ya mama yangu mkubwa yalionekana kunigusa sana.
Niliomba msamaha na mke wangu alinisamehe bila hiyana.
Siku hiyo ilikuwa ni msiba mwingine mara baada ya kifo changu.
Usiku huo watoto wetu walilala kwa amani kabisa.
Usiku nilikuwa na kazi ya kumuomba mke wangu msamaha sikuamini kama alikuwa amenisamehe.
Kila wakati nilikuwa nikimuomba anisamehe na yeye alinihakikishia kwamba amenisamehe na ananipenda sana.
“Nakupenda sana Mudi.”
Alisema Aisha.
“Nakupenda pia mke wangu. Leo nimejua thamani yako kwangu naomba nishamehe sana.”
Kila baada ya sentesi moja nilikuwa nikiweka neno nisamehe.
Nililala kifuani kwake alinibembeleza mpaka nilipopitiwa na usingizi.
Niliamka asubuhi nikiwa na uchovu sana.
Siku hiyo nilipania kwenda kazini kwangu kujionesha.
Mke wangu aliniandalia chai aliniandalia maji ya kuoga pamoja na nguo kwa upendo mwingi.
Niliondoka na kisha kuelekea ofisini kwangu.
Kila mmoja aliponiona alikimbia.
Walidhani wamemuona mzuka.
Hata mara baada ya kuwahakikishia utulivu ulirejea.
Bosi aliita kikao cha dharula na kisha nilipewa nafasi ya kuongea kila kitu.
Wala sikutaka kuficha chochote niliongea ukweli wote na hata hali niliyoikuta nyumbani.
Kila mtu alinihurumia sana.
Bosi nae pia aliomba msamaha kwaajili ya wafanyakazi wote kwa kushindwa kuhudhuria msibani.
“Hatukuona umuhimu bwana mara baada ya kusikia kwamba miili yote inazikwa kule.”
Hata hivyo siku hiyo nilipewa ruhusa ya wiki nzima ili nikae nyumbani.
Nilirudi nyumbani na kisha kuendelea kuishi vizuri na mke wangu.
Kila mara mke wangu alikuwa akinikumbusha kuhusu swala la kuwasamehe ndugu zangu.
Kiukweli iliniwia vigumu sana niliona ni wasaliti wakubwa kwangu.
Mara baada ya kunishawisi kwa muda mrefu na mke wangu ambaye kwa wakati huo nilimuona ndiyo kiumbe pekee ambacho
ninaweza kukiamini hapa duniani.
Niliwasamehe hata hivyo sikutaka kuwa na ukaribu nao kivile.
Kila mara dada yangu alikuwa akimpigia mke wangu simu na kumuomba msamaha.
Nilimuonya asijaribu kuisogelea familia yangu.
Nilimuonesha mke wangu miradi yote huku nikimpa wajibu wa kusimamia maduka yetu.
Na sasa hakuwa tena mwanamke wa nyumbani.
Aliweza kuisimamia miradi yetu vizuri na ndani ya muda mfupi iliweza kuleta faida nyingi sana ambapo tuliweza kupanua
maduka yetu pamoja na kuongeza mengine.
Nilimuamini sana mke wangu tangu hapo na tuliishi kwa furahaaaa……
Maisha yetu yote.
***** MWISHO *****
Unaweza pia kusoma: