Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

High School - Episode 02

Ilikuwa ni siku ya Ijumaa siku niliyowahi kuamka tofauti na kawaida nilimshuhudia Candy akivaa mkanda wa kupunguza tumbo nilijiuliza maswali bila majibu mkanda wa nini na hakuwa na tumbo.
Huku nikijifanya nimelala niliendelea kumtazama wakati akivaa.
“Ili tumbo mwishowe litaniumbua, looh!”
Alijiongelesha mwenyewe.
“Leo lazima huyu kidudu mtu anipe mustakabali wangu kabla mambo hayajawa mabaya.”
Aliongea.
Nilichelewa kugundua kuwa Candy ni mjamzito.
Aliendelea kujiandaa na kisha alijongea kabatini kwake.
Alipofika kwenye meza ya kujisomea mahali nilipoweka daftari zangu na vitu vyangu alisita, alichomoa kitambaa ambacho hata kwangu kilionekana kipya sikuwa nimewahi kuwa na kitambaa cha namna hiyo nilijiuliza kimetoka wapi na cha nani na kimefikaje kwangu, bila majibu.
Candy alikitazama, akasonya na kisha akakirudisha kilipokuwa na kisha akaliendea kabati lake.
“Candy.”
Sauti ilipenya kwenye masikio yangu, alikuwa ni msichana mwingine ambaye nilizoea kumwona pale shuleni ambaye alikuwa akiitwa Naima alipenda kujiita Nana.
“Niambie best yangu.”
Candy alijibu.
“Meseji yako nimeiona leo asubuhi nikaona nije sasa hivi kabla ya kuingia darasani.”
Alisema Naima.
“Ndio hivyo shoga yangu.”
Candy alijibu.
“Sasa itakuwaje?”
Naima aliuliza.
“Nataka nimfate Maloya anipeleke nikaitoe kwa maana imeshafikisha miezi miwili, mwisho wake tumbo litakuwa kubwa itajulikana hali itakuwa mbaya zaidi.”
Kijasho chembamba kilinitiririka kumbe Candy ana uhusiano na Maloya uhusiano uliozaa mimba na sasa wanampango wa kuitoa hiyo mimba, duuh! Nilichoka.
Waliendelea na maongezi yao hadi walipofikia muafaka kuwa Candy aende kwa Maloya ampeleke kuitoa hiyo mimba.
“Huyu kiazi ajasikia kweli?”
Aliongea Naima kwa dharau.
“Mmmh, linalala kama ling’ombe.”
Candy alijibu kwa nyodo wakacheka na kisha wakatoka.
Niliendelea kuwaza pale kitandani, Candy kwanini umefanya hivyo jamani we ni msichana mzuri kwanini unajiaribia uzuri wako niliwaza.
Ni kweli Maloya alikuwa kijana tena mzuri alikuwa ni mwalimu mzuri sana na zaidi ya yote alikuwa na haiba nzuri, lakini Candy ni kwanini ukaingilia mambo haya wakati sio wako.
Ona sasa umepata ujauzito na sasa unataka kuhatarisha maisha yako kwa kutoa huo ujauzito.
Niliendelea kuwaza pasipokuwa na majibu.

Nilikuja kushituka wakati umeshaenda na nilikuwa nimeshachelewa sana niliamka na kujiandaa kwa haraka na kukimbilia darasani muda wote nilionekana mtu mwenye mawazo sana, Martha aliligundua hilo na Martin pia, kila mmoja aliniuliza kwa wakati wake.
Nilimjibu Martha sina tatizo.
“Martin ninaomba mda niongee na wewe.”
Nilimwambia Martin.
“Aaanh sawa tutaongea wakati wa mapumziko.”
Alinijibu kwa sauti yake nzuri.
Kiukweli nilishindwa kuvumilia kuyabeba mambo ambayo niliyasikia asubuhi ya siku hiyo niliona ni vema kumshirikisha Martin kwa sababu nilikuwa nikimuamini na alikuwa rafiki yangu wa karibu sana.
Wakati wa mapumziko hatukwenda kula tulibakia darasani.
“Martin.”
“Nakusikiliza bibie.”
Martin alijibu.
“Unafahamu kwamba naishi na Candy chumba kimoja?”
“Ndiyo najua.”
Alisema.
“Kiukweli nimejua kitu ambacho binafsi kimenichanganya sana na nimeshindwa kuvumilia kukaa nacho nimeona bora nikushirikishe”
“Niambie kitu gani hiko?”
Alisema Martin.
“Candy ni mjamzito.”
Martin alishituka isivyo kawaida tofauti na nilivyo tegemea.
“Say whaaat!?”
Alisema kwa ghadhabu.
“Martin candy ni mjamzito.”
“Huweza kuwa serious Catherine, kwanini unaongea utani?”
Aliniuliza.
“Hapana sio utani nina uhakika na hilo.”
Alishindwa kuendelea alibakia akitweta huku jasho jembamba likimtiririka.
“Na ana mpango wa kuitoa.”

Niliendelea.
Hakujibu aliendelea kujiinamia pale chini.
“Kibaya zaidi.”
Niliendelea.
“Ujauzito huo ni wa mwalimu Maloya.”
Martin aligeuka na kunitazama kwa jicho kali.
“Unaongea nini wewe?”
“Martin huamini ninachokuambia?”
Niliongeza.
“Katika siku ambayo umewahi kunichanganya leo ni siku ya kwanza sitaki kukuamini Catherine sitaki kabisa.”
Alisema Martin kwa sauti ya kukata tamaa.
“Martin nina uhakika na ninacho kiongea.”
“Kumbe ndo mana candy amebadilika sana siku hizi aonekani darasani hataki tena kuja kuniona naa…”
Ni kama alishitushwa na akaishia hapo.
“Ok sawa nitalifanyia kazi kwaheri Catherine.”
Aliondoka Martin mbele yangu, nilitamani kumwita lakini nilishindwa nilijua kutokana na yeye kuwa ni raisi wa shule lazima ingemchanganya lakini sio kwa kiwango kama hicho.
Ana nini huyu Candy anamhusu vipi?
Nilijiuliza maswali bila majibu.

Mwisho wa yote niliendelea kukaa darasani kwa ajili ya vipindi Martin hakurudi tena, vipindi vilipoisha nilirejea bwenini kwetu. Nilipoingia chumbani kwangu nilimkuta Naima na Candy wamesimama kana kwamba wanamsubiri mtu kisharishari nilisita nikaingia na kisha nikawasalimia mambo zenu, hawakunijibu.
Nilishangaa kwani kuna tatizo lolote niliuliza hawakunijibu baada ya kukosa majibu niliamua kuendelea na mambo yangu, nikasogea mezani kwangu kwa ajili ya kuweka madaftari yangu.
Candy alinisukuma.
“Wewe ndiyo unaejifanya mzuuuuri kuliko wote hapa shuleni kiasi cha kuchukua wanaume za watu unajiamini nini na kwa uzuri gani, unanitafta nini wewe kidudu mtu, eeenh.”
Aliongea Candy kwa hasira zenye mchanganyiko wa jazba.
Nilishindwa kumuelewa nilibaki nimetoa macho huku nimeachama mdomo.
“Candy sielewi unaongea nini?”
Nilisema.
“Uelewi naongea nini?”
Candy aliongea huku amenibania pua.
“Mpumbavu sana we msichana umefika hapa shuleni unaanza kujiona wewe ni mzuri umeshazoea shule kiasi unaingia anga za watu nataka nikwambia kwamba hapa umekalia kuti kavu.”
“Candy unanichanganya sijui unaongea kuhusu nini mbona sikuelewi kwani nimekufanya nini mimi?”
“Hujui ee hujui unajifanya hujui.”
Alidakia Naima.
“Usione tumekunyamazia kimya tunakuogopa tunakuchora tu maana umekuja hapa unataka kujifanya wewe staaa eee.”
Walizidi kunichanganya nilishindwa kuwaelewa.
“Candy kama hutaki kunielezea ni nini kimetokea mimi sikuelewi na siwezi kuendelea kukusikiliza nina mambo mengi ya kufaya nielezee tatizo ni lipi ili mi nijue tatizo likowapi, sasa unaniambia tu unaniongeleshaongelesha mi vitu sivielewi nashindwa kukuelewa.”
Niliongea kwa kupaniki.
“Unashindwa kunielewa?”
Alichukua leso ambayo ilikuwa katika madaftari yangu pale juu.
“Hii leso umeipata wapi unajua imetoka wapi hii wewe eee?”
Haaa!
Nilishangaa.
“Hiyo leso hata sijui kwangu imefikaje.”
Niliongea huku nikionesha kutojiamini.
“Hiyo leso hata sijui kwangu imefikaje.”
Aliongea huku amebana pua zake, nilibaki tu nimeshangaa.
“sikia nikwambie kaa mbali na wanaume za watu.”
Nilijiuliza maswali yaliyokosa majibu, Maloya ameweka wapi leso yake kwenye madaftari yangu na ni lini?, nikabaki najiuliza.
Waliendelea kunipasha na kunipashua.
Sikutamani kuendelea kuwasikiliza, nilijawa na mawazo mengi sana, waliongea, walinisema na matusi makali ya nguoni walinitukana waliporidhika walicheka kwa dharau na kisha wakatoka.
Nilipanda kitandani kwangu nikiwa mnyonge na mwenye mawazo mengi, nililia sana, nililia mno.
“Nimekosa nini mimi, toka nimefika hapa shuleni sina hata miezi miwili tayari nimeshaanza kukutana na mambo ya ajabu kama haya nitaweza kweli, Maloya kwanini umenisababishia matatizo hivi uliweka vipi leso yako katika madaftari yangu ona sasa jinsi nilivyotukanwa, mungu nisaidie, nililia kwa uchungu.”

Nililia hadi nilipopitiwa na usingizi nilikuja kuamka tayari ilishakuwa jioni, nilihisi njaa lakini sikuwa na hamu ya kula kabisa.
Nilioga na kisha nikatoka kwenda darasani sikutamani hata kuhudhuria kwenye kipindi cha dini cha siku hiyo nilikuwa na mawazo mengi sana, nilipoingia darasani nilishindwa kujisomea, nilikuwa mnyonge sana niliendelea kuwaza na kuwazua pasipo majibu.
“Cathe.”
Martin aliniita niligeuka na kunitazama kisha nikaendelea nikarudisha macho yangu chini alivuta kiti na kukaa pembeni yangu.
“Cathe unaonekana mnyonge sana leo, unaumwa?”
Aliniuliza kwa upole.
“Hapana siumwi niko salama.”
Niliongea kana kwamba nimelazimishwa.
“Unaonekana hauko sawa any way kama huoni umuhimu wa kuniambia sawa.”
Niliinama pasipo kumjibu lolote.
“Cathe nataka nikwambie kitu.”
Aliongea.
“Nilipofika hapa shuleni nilikuwa nikisumbuliwa sana na wasichana, wengi walikuwa wakinitaka kimapenzi lakini nilikataa kwa vile sikutaka kuwa nao yote kwa yote nilishindwa kwa mtu mmoja tu sio kwa sababu ya kwamba yeye ni mzuri au kwa sababu alikuwa na kila kitu ambacho nilikuwa na kihitaji au kwasababu alikuwa na pesa ila kwasababu alitumia nguvu kuniforce.
Muda mchache wa mapenzi yetu nilijikuta nampenda sana.”

Aliongea kwa hisia kali zenye kugusa moyo niligeuza macho yangu na kumtazama.
“Eeeehe..”
Nilimwambia huku nikionesha utayari wa kuendelea kumsikiliza.
“Alitumia nguvu sana kuniforce sikuwa na jinsi kwa maana alitumia hadi vitisho kwa vile mimi na yeye hatutokei mkoa mmoja niliona atakuwa akinisumbua sijui ni nini kilinifanya najikuta nampenda hivi, vituko vyake vilinichosha.
Maisha yaliendelea lakini alikuwa akionekana akibadilika sana kitabia nilichoka kumvumilia, nikampa uhuru afanye kile anachokitaka, niliendelea na maisha yangu.
Siku akinimisi alikuwa akija kwa mbwembwe nyingi, vizawadi na ahadi kemukemu, alikuwa anajishaua mbele yangu, nilikuwa nikimwonesha ushirikiano kwasababu yeye ni mtoto wa kigogo mkubwa sana baba yake ndiye anamiliki hii shule alikuwa akinitishia kunifukuzisha shule mara kwa mara wazazi wangu walikuwa wakinihusia sana kuhusu kusoma, kwasababu wanatoa hela nyingi sana kunilipia ada hapa shuleni hivyo walikuwa hawapendi nifanye ujinga hapa shuleni nilitii amri.
Kiukweli taarifa yako imeniumiza sana sitaki kuamini kwamba Candy wangu alikuwa anatembea na Maloya kiasi cha kubeba mimba.”

Nilishituka, nikajikuta nimetoa macho, nilishtuka pasipo na kifani.
“Martin unaongea nini?”
Nilimuliza kwa sauti darasa zima waligeuka na kutuangalia.
“Aaanh sorry class mnaweza mkaendelea kusoma.”
Niliongea kwa woga Martin alitikisa kichwa pasi na kuniangalia.
“Ndivyo ilivyokuwa Cathe.”
Nilishusha pumzi za uwoga.
“Inamaana wewe ndiyo uliweka leso yako kwenye madaftari yangu.”
Aligeuka kwa haraka na kuniangalia.
“Sijaiyona leso yangu leo nina siku ya pili, ni leso ambayo alinipatia Candy.”
“Ooh my god kumbe.”
Nilionge.
“Nimetukanwa sana na Candy kisa hiyo leso nilijua ni leso toka kwa Maloya sikujua kama una mahusiano na Candy samahani kwa kukuletea taarifa mbaya.”
Niliongea nilinyanyuka na kusimama, alinivuta mkono.

“Martin sikuwahi kujua kama uhusiano wangu na wewe utaleta shida nimekuja hapa kwa ajili ya kusoma sio vitu vingine tazama nimeanza kugombana na watu kisa ni wewe endelea na Candy wako na mimi niache nisome.”
Nilisema kwa hasira lakini kwa upole wa ajabu chozi likinitoka.
“Candy yupi sasa?”
Ailiniuliza kwa kutojiamini.
“Candy mwenye ujauzito wa mwalimu na bado unasema Candy wangu.”
Nilishindwa kuongea nilimwonea huruma sana.
“Pole kwa kilichokukuta Cathe.”
“Asante.”
Nilisema kwa upole.
“Yaliyotokea yamesha tokea la muhimu ni kujua nini kinachofuata nashukuru mungu sihusiki na ujauzito wa Candy.”
Aliongea lakini kwa sauti iliyoonesha kukata tamaa.
“Martin kuna tatizo zaidi ya hili?”
“Ndio tatizo lipo…
Nilijua ni kwa nini Candy alinitakaa mimi na hakupenda uhusiano wetu uwe wazi.”

“Kwa nini.?”
Niliuliza.
“Anataka kunitumia mimi kama chambo endapo tatizo litakuwa kubwa.”
“Unamaanisha nini?”
“Ninamaanisha huo ujauzito utakapogundulika Candy atanitaja mimi na sio Maloya.”
“Huuu..”
Nilishusha pumzi ndefu.
“Pole Martin.”
“Sijapoa na sitapoa mbele yangu naona giza kubwa sana.”
Nilijutia kiherehere changu cha kwenda kumwambia Martin kuhusu Candy.
Nilishindwa nimwambie nini mtoto wa watu aliyekuwa mbele yangu amekata tamaa.
“Martin nitakuwa bega kwa bega na wewe nitahakikisha kwamba hakuna kitu kibaya kinatokea kwako, nitakupigania kadri ya uwezo wangu naomba usikate tamaa wala usijifikirie vibaya kuhusu Candy nitasimama upande wako.”
Niliongea kwa kujiamini zaidi, aliniangalia, akaachia tabasamu la uchungu.
“Aaahh sawa.”
Nlisema.
“Ok.”
“Tuendelee kusoma.”
Nilisema.
“Sina mood wa kusoma kabisa.”
Alisema.
“Mimi pia.”
“Basi tupige story nyingine.”
Tuliendelea kupiga story nyingine mpaka mda wa prepo ulipoisha aliomba kwenda kupumzika na mimi nilielekea chumbani kwajili ya kupumzika.

Sehemu 1 Sehemu 3
0
0