High School - Episode 05 
Tulipendana sana huku tukishirikiana katika mambo mbalimbali pale shuleni.
Alikuwa mshauri wangu mkubwa na pia tulishirikiana kimasomo ili kuhakikisha kwamba tunafanya vizuri katika mitihani yetu.
Ukizingatia wakati huo tulikuwa tumebakiza wiki chache tu kufanya mitihani yetu ya muhula wa pili.
Candy mahusiano yetu yalimuumiza sana.
Alizidi kunipa adhabu mbalimbali lakini sikujali kwakuwa kwa wakati huo hakuwa akinionea tena.
Mahusiano yetu yalizidi kustawi ingawa ndani ya nafsi yangu sikuwa na amani, kisasi juu ya baba kilinisumbua sana
mara zote nilitamani kumlipizia kisasi.
Niliwaza sana nitakaporudi nyumbani lazima nilipize kisasi kwa baba haiwezekani kuniulia mama yangu.
“Haiwezekani baba lazima ulipe damu ya mama yangu.”
Niliwaza.
Martin alikuwa akinishauri sana kuhusu swala la kulipiza kisasi.
“Achana nayo yameshapita hata ukilipiza kisasi mama yako hatoweza kurudi mwache msamehe baba.”
Alikuwa akinishauri.
Nilifanya kama namemuelewa ingawa nafsi yangu ilikataa kabisa kuendana na mawazo yake.
“Lazima nikalipize kisasi.”
Nilisema.
Tulifanikiwa kufanya mitihani yetu ya mwisho na kufaulu kwa ufaulu mzuri kabisa.
Tulirudi nyumbani mimi na Martin tulikuwa tukitokea Dar es salaam.
Candy alikuwa akitokea Arusha hivyo naye alielekea kwao ingawa kwa masikitiko sana alikuwa akiumia sana kumpoteza Martin.
Wakati wa likizo tulitumia muda mwingi sana kuwa pamoja mara nyingi tuliongozana sehemu mbalimbali za burudani.
Nilipata amani na furaha sana moyoni mwangu kuwa pembeni ya Martin wazo langu la kulipiza kisasi bado nilikuwa nalo.
Mara nyingi baba hakuwepo nyumbani nilikuwa nabaki peke yangu, toka nimerudi likizo baba alikuwa akichelewa sana kurudi nyumbani
na akiwahi sana kuondoka.
Mara chache sana nilikutana na baba yangu na hakuwa katika hali ya kawaida.
Kila mara nilikuwa nikimshangaa jinsi alivyo baba alivyobadilika sana.
Nilipanga lazima tu nilipize kisasi kwa namna yoyote ile ingawa hadi wakati huo sikuwa naijua ni kwa namna gani nitalipiza
kisasi.
“Siwezi kumuua baba yangu.”
Nilisema.
Muda mwingi niliutumia kuwa na Martin na wakati huo niliweza kupoteza usichana wangu.
Martin aliniingiza katika dunia ya mapenzi sikujali kuhusu hilo ingawa mama yangu alikuwa akinihusia sana kuhusu
kujitunza sikuona umuhimu wowote kwasababu mama yangu mwenyewe hakuwepo duniani niliona ni kawaida.
Mapenzi kati yetu yalizidi kuongezeka hata hivyo akili yangu ilikuwa ikifikiria vitu vingine kabisa.
Muda ulienda na wakati wa kurudi shuleni ulikaribia.
Nilichelewa kuona kwamba sijafanya kisasi kwa baba yangu niliamua kwa muda huo mchache lazima niwe nimefanya kitu,
kama kawaida yake baba alichelewa sana kurudi nyumbani na aliwahi kuondoka asubuhi.
Alipotoka tu nilinyatia hadi chumbani kwake, nilipoingia nilishangaa kukuta baba hafungi chumba chake siku hizi.
Nilikuwa naogopa sana kuingia chumbani kwa baba yangu enzi za uwepo wa mama.
Mara zote sikuruhusiwa kuingia bila ruhusa maalumu niliingia mara chache sana.
Nilikuwa nikitetemeka mno kuingia chumbani kwa baba.
Mazingira niliyokutana nayo pale chumbani yalinishitua sana, palikuwa ni pachafu kana kwamba haishi mtu.
“Nahisi toka mama amefariki hiki chumba hakijawahi kufanyiwa usafi.”
Niliwaza.
Nilipofika katikati ya chumba nikasimama.
“Nafanya nini humu sasa?”
Nikajiuliza.
“Humu ndio nimekuja kulipiza kisasi kwa baba yangu?”
Nilibaki nimesimama nisijue nini cha kufanya.
Ghafla nikaijiwa na wazo la ghafla nikaenda kwenye droo ya baba yangu na kuanza kufungua fungua droo moja baada ya nyingine.
Nilikuwa nafungua tu nisijue nini natafuta.
Katika kupekua pekua nilikutana na vyeti vya hospitali vingi, moyo wangu ulinishawishi kuviangalia.
“Aaaah! mimi si nimekuja kwaajili ya kulipiza kisasi? Hivi vyeti vya nini? Mimi naachana navyo bwana.”
Nilijiwazia, upande wa pili nafsi yangu iliniambia nivifuatilie.
Nikaviweka kitandani kisha nikaanza kukagua kimoja baada ya kingine.
Moyo wangu ulizimia cheti cha kwanza kukiona kilikuwa ni cha marehemu mama yangu.
Ilikuwa ni ripoti ya daktari kuhusiana na kifo chake ambayo sikuwa na shaka kuwa haikusomwa siku ya msiba wake.
Mama yangu alikufa kwa stroke (kiharusi).
Na hii imetokana na kupasuka kwa mirija yake ya damu kutokana na kipigo kikali alichokipokea kutoka kwa baba.
Hadi kufikia mwisho ripoti ya daktari machozi yalikuwa yakinitoka huku mwili mzima ukitetemeka.
Nilijawa na hasira mara mbili yake nilitamani baba awepo karibu yangu nichukue hata kisu nimchome aondoke mbele ya macho
yangu sikumpenda kabisa.
Nikasimama ili niondoke nikagundua kuna vyeti vingine ambavyo vimebakia hapo chini nilivichukua huku mikono ikitetemeka
na kuanza kuvisoma.
“Mungu wangu!”
Nilisema.
Vilikuwa ni vyeti vya baba yangu kutoka katika hospital maarufu sana hapa mjini.
Vilikuwa vikionesha kwamba baba yangu yupo katika hatua za mwanzo za kansa ya ini na hii imetokana na ukweli
kwamba baba yangu alikuwa mlevi kupindukia hasa mara baada ya kifo cha mama.
Nililia sana ni sawa nilikuwa nikimchukia baba yangu lakini kujua kwamba baba yangu ana kansa ya ini na asingekuwa
na maisha marefu iliniuma sana wazo la kisasi lilipotea kabisa katika moyo wangu.
“Kwanini mimi? Kwa nini matatizo hayaniishi?”
Nililia mno.
“Baba ukiondoka nitabaki na nani sasa?”
Nilitoka chumbani kwa baba nikawa nimenyong’eya nilijutia kiherehere changu kutaka kulipiza kisasi bora nisingejua
nililia siku nzima sikutaka hata kuongea na Martin na mtu mwingine yoyote nilijifungia chumbani siku nzima.
Nilikuja kusituka ni asubuhi yake Martin alikuwa amekuja nyumbani alikuta mlango uko wazi akaingia moja kwa moja hadi chumbani kwangu.
“Cathe kwanini hupokei simu yangu wala hujibu meseji zangu?”
Aliniuliza.
“Hapana hamna kitu.”
Nilisema.
“Kuna tatizo? kama lipo naomba niambie.”
Aliniuliza.
“Hapana hakuna tatizo lolote.”
“Sikupenda ajue.”
Tulishinda wote hadi ilipofika jioni.
Jioni baba aliporejea alitukuta na Martin mara nyingi alizoea kutukuta na Martin nyumbani, alisalimia pasipo
uchangamfu na kupitiliza chumbani kwake.
Sikuweza kupata muda wa kuongea na baba muda mwingi alikuwa akinikwepa.
Wakati wa kurudi shuleni ulipofika nilirudi shuleni kinyonge sana.
Martin alikuwa akiniuliza mara kwa mara.
“Kwanini umepoteza uchangamfu wako Cathe.”
Aliniuliza.
“Hapana usijali.”
Nilisema.
Ingawa hata ndani ya nafsi sikuona kama nipo kawaida nilihisi nina kitu ndani yangu sikujua ni kitu gani.
Nilirudi shuleni nikiwa na unyonge sana.
Safari hii Candy alikuwa amenipania sana sikuogopa kitu.
Martin alizidi kunipenda na tulizidi kudhihirisha uhusiano wetu, haikuwa siri tene pale shuleni.
Tatizo na lenye kuumiza kuliko yote lilijitokeza.
Chuki ya Candy ilizidi juu yangu pamoja na faraja niliyokuwa naipata kutoka kwa wanafunzi na kwa baadhi ya marafiki zangu
Martin akiwa mmoja wapo haikutosha kunifanya nisiogope.
Niliingiwa na woga sana kwa sababu alikuwa akinitisha mara kwa mara nilipokea meseji za vitisho kutoka kwake mara nyingi
akiniambia kwamba atanifanyia kitu kibaya, nilianza kuogopa sana.
Martin aliweza kunitia moyo na mara nyingi alikuwa akinisisitizia kuwa makini, nilijaribu kujiweka busy na masomo
na kumtoa Candy katika akili yangu.
Sikutaka kurudia makosa niliyoyafanya hapo kabla, nilitamani kufanya vizuri katika mitihani yangu ya mwisho hivyo sikupaswa
kurudi nyuma tena.
Siku moja niliitwa ofisini kwa mwalimu Maloya niliogopa sana kwenda ingawa sikuwa na jinsi kila nilipokuwa nikipiga
hatua moyo wangu ulikuwa mzito nafsi ilinishauri sana nisiende ingawa upande mwingine uliniambia niende.
Laiti ningejua nisingeusikiliza upande huu.
Nilipiga hatua zangu za kinyonge hadi ofisini kwa Maloya nilipoingia hakunikaribisha kama ilivyokuwa siku zote,
niliingia na kubaki nimesimama.
“Shikamoo mwalimu.”
Nilimsalimia hakunijibu.
“Nimeitikia wito.”
Nilimwambia bila kujali jinsi ambavyo alikuwa amechukia.
Alisimama.
“Karibu binti mrembo, mrembo ambaye unajisikia unajiona mzuri kuliko wote hapa shuleni.”
Aliongea kwa dharau.
Unamaanisha nini mwalimu.
“Hivi we unafikiri ni mzuri sana kiasi cha kinikatalia mimi?
Wasichana wenzio wazuri kabisa kama wakina Candy hawaringi kama unavyoringa wewe, wewe ni nani hasa?”
Nilishindwa kumwelewa.
Akili ilianza kuniambia kuwa tukio baya litatokea.
Miguu iliniwia mizito sana kuondoka.
Nilitamani kukimbia lakini nguvu zilinishia.
“Wewe ni mtoto mdogo sana huwezi kunishinda mimi alaaa!”
Alisema na kusogea pale nilipokuwa.
Nilisimama kujizatiti kwa ajili ya kile kilichokuwa mbele yangu.
Alikuja hadi mbele yangu akasonya kisha akinipita alielekea mlangoni.
Nilijua alikuwa akienda kuchukua fimbo kwa ajili ya kuniadhibu.
Adhabu nilishazizoea nilikuwa tayari aniadhibu.
Maloya alifika mlangoni na kujifanya kama anachukua fimbo akafunga mlango na kisha akanigeukia.
“Leo utaongea na mimi.”
Akanisogelea.
“Unanikubali hunikubali?”
Aliongea kwa ghadhabu.
“Hapana mwalimu siko tayari.”
Niliongea kwa sauti ya chini sana.
“Utanipa hunipi?”
Nilishituka.
“Hapana mwalimu siwezi kukupa.”
“Siwezi kukupa unachotaka naomba niruhusu niondoke.”
“Huendi popote leo Cathe ama zako ama zangu.”
Alinishika kwa nguvu na kufanya kile ambacho alitarajia kufanya.
Nilihisi maumivu makali sana ndani ya moyo wangu.
Sikutegemea mtu ambaye nilikuwa nikumheshimu kama mwalimu na mlezi wangu katika mazingira kama haya
angenitendea kitendo hicho.
Maloya alinibaka bila huruma nililia sana, alinizidi nguvu nilishindwa kujiokoa nilijaribu kupiga kelele aliniziba mdomo.
Baada ya kutekeleza unyama huo alivaa nguo zake.
“Vaa uende bwana, unaringa nilijua unajitunza kumbe na wewe hamna kitu ondoka.”
Aliniongea kwa dharau.
Moyoni mwangu niliumia sana.
“Unajifanya mlokole kumbe huna lolote wajanja washa kuchezea wewe toka bwana.”
Aliongea.
Nilivaa nguo zangu kiunyonge sana na kupiga hatua za kinyonge kuelekea mlangoni.
“Cathe.”
Aliniita.
“Ole wako unyanyue mdomo kumwambia mtu yoyote nitakuua.”
Alisema.
Niliondoka kinyonge kuelekea bwenini nilifunga mlango na kuanza kulia Nililia sana.
“Kwanini matukio haya yote yananitokea mimi tu ina maana hamna mtu mwingine wa kushea na mimi shida hizi.
Kwa nini mimi peke yangu.”
Nililia sana.
“Kwanini haya yote.”
Nililia.
Nililia mpaka nilipopitiwa na usingizi nilikuja kushituka ilikuwa jioni sana.
Sikusikia hamu ya kula wala kutoka kwenda sehemu yoyote.
Nilibaki hapo kitandani hadi siku ya pili yake.
Sikujisikia kuingia darasani, nilibaki tu nimelala sikuwa na hamu ya kula nilikula tu pale nilipohisi njaa,
hali hiyo iliendelea kwa wiki nzima.
Martin alikuwa akinitafta kila kona huku walimu wakiulizia ni wapi nilipo.
Nikiwa bwenini niliwaza haya yote yatakwisha lini ndani ya nafsi yangu.
Niligundua ni lazima niyachukulie kama sehemu ya maisha yangu.
Lazima niwe na amani sasa.
Kujua kwamba nimezaliwa ili niteseke, nilizaliwa ili nipate uchungu, kamwe haikuniumiza katika maisha yangu.
Nilijitia moyo sana kwamba hayo yote ni maisha yangu ambayo nimeletwa nije niishi.
Hakika nilipata faraja kubwa sana na kwa wakati huo niliapa sitolia tena, kwa sababu hayo ni maisha yangu
Mungu amenileta ili niyaishi.
Nilitoka bwenini na kisha kuelekea nyuma ya shule.
Martin aliniona na kunifuata.
“Cathe kwanini huingii darasani wiki nzima , una nini?
Una unaumwa?
Kwanini uko hivyo Cathe kwanini lakini?”
Aliuliza maswali mfululizo ambayo nilishindwa kujibu.
“Aaah Martin uwe na amani niko sawa kabisa.”
“Nakujua vizuri kama una tatizo ni bora uniambie ili nijue ni nini naweza kukusaidia.”
Sikutaka kumwambia sikutaka ajue, ningewezaje kwanza kumwambia.
“Hapana hakuna kitu.”
Nilihisi machozi yanaanza kunitoka nilinyanyuka pole pole na kumwacha Martin peke yake pale.
Niliondoka na kuelekea bwenini jioni ya siku hiyo niliamua kuingia darasani.
Nikiwa na furaha kwa kujua kwamba matatizo ni sehemu ya maisha yangu nilingia darasani kwa bashasha zote.
Nilikutana na Martin tukasalimiana kwa uchangamfu tukaketi.
“Nilikumis sana Cathe, ingawa hutaki kuniambia tatizo lilikuwa ni nini.”
Nilicheka.
“Martin sina tatizo lolote uwezi kuniamini mimi mpenzi wako.”
Alitabasamu.
“Nakuamini mke wangu mtarajiwa.”
Alisema.
Nilicheka.
Tukacheka kwa pamoja kisha tukaendelea kusoma.
Siku hiyo ilipita kana kwamba hakuna kilichotokea, maisha yaliendelea.
Unaweza pia kusoma: