Faida za kufanya mapenzi au kufanya tendo la ndoa ukiwa mjamzito
Ikiwa unatarajia kuongeza mtu katika familia yako kuna mabadiliko mbalimbali ambayo unaweza kuyaona kwako au kwa mpenzi wako.
Kuna baadhi ya shughuli ambazo itakupasa kuziacha au utashauriwa kuziacha lakini tendo la ndoa si moja ya shughuli hizo.
Ni salama kabisa kwa mjamzito kufanya tendo la ndoa katika kipindi cha ujauzito, isipokuwa tu kama utaona chupa imepasuka au majimaji mepesi ambayo si kama mkojo yanatoka ukeni au kama utashauriwa vinginevyo na wataalamu wa afya kuachana kabisa na tendo la ndoa.
Mjamzito usifanye mapenzi au tendo la ndoa kama ukiona mambo haya
Katika kufanya tendo la ndoa ukiwa mjamzito epukana na staili mbalimbali ambazo ni hatari wakati wa ujauzito, kama vile kulalia mgongo kwa muda mrefu au staili inayoweza kusababisha kuminya tumbo.
Licha ya kuwa kuna baadhi ya hatua katika kipindi cha ujauzito mjamzito anapata hamu sana ya tendo la ndoa pia tendo la ndoa lina faida kadhaa kwa mjamzito. Kufanya mapenzi wakati wa ujauzito kunaweza kuwa na faida kwa mjamzito na kwa mwenza wake pia, faida hizo ni kama ifuatavyo.
Kuimarisha mahusiano yenu na mpenzi wako:
Faida nyingine ya tendo la ndoa kipindi cha ujauzito inasaidia kuimarisha mahusiano yenu katika ndoa.
Kuongezeka kwa raha zaidi wakati wa tendo kuliko kawaida:
Katika kipindi cha ujauzito damu nyingi hushuka kwenye viungo vya uzazi kwa mwanamke, hiyo inasaidia kuongeza raha zaidi unapofika kileleni.
Kuweka mwili imara:
Tendo la ndoa pia husaidia kuufanyisha mazoezi mwili kuwa imara pia inasaidia kupunguza mafuta mwili ambayo yanaweza kusababisha kupanda kwa shinikizo la damu au presha, ambayo ni hatari wakati wa ujauzito.
Kuimarisha kinga ya mwili:
Baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa tendo la ndoa husaidia mwili kuzalisha kinga za mwili ambazo husaidia kukukinga na kifua na magonjwa mengine ya kuambukiza, hivyo kukuweka salama kipindi cha ujauzito.
Kuongeza furaha na kuondoa msongo wa mawazo:
Wakati wa tendo la ndoa mjamzito anapofika kileleni mwili huzalisha homoni ya endorphins ambayo husaidia kumpa furaha mama mjamzito na mtoto wake tumboni, pia husaidia kuondoa msongo wa mawazo.
Unaweza pia kusoma: