Ukuaji wa mtoto tumboni kwa mama mjamzito mwenye mimba ya miezi saba.
Mimba ni mchakato wa asili wa muda mrefu kwa binadamu, inachukua takribani siku 280 au wiki 40 ambayo pia inakadiriwa miezi 9 mpaka mtoto kuzaliwa na kuwa na uwezo wa kuyaishi mazingira ya nje ya tumbo la mama.
Mchakato huu kwa mtoto huanzia kwenye seli moja tu ambayo ni mchanganyiko wa yai la mama na mbegu ya baba.
Seli hiyo hugawanyika mpaka kupata mamilioni mengine ya seli ambazo huunda viungo mbalimbali ndani na nje ya mwili wa mtoto.
Kuna hatua mbalimbali ambazo mtoto tumboni anazipitia kutoka yai la mama kurutubishwa mpaka wakati wa kujifungua.
Tufahamu nini kinachoendelea tumboni kwa mama mjamzito katika miezi yake yote 9 mpaka kujifungua.
Ukuaji wa mtoto tumboni kwenye mwezi wa saba unaongezeka kwa kasi mpaka mtoto kufikia urefu wa nchi 14 mpaka 16.
Uzito wake pia unaweza kufikia kilo 1 mpaka kilo 1 na nusu.
Mwili unakuwa umezalisha mafuta ya kutosha kiasi cha kupunguza mikunjo ya ngozi ya mtoto.
Mfuta hayo pia yanasaidia kupevusha viungo vya mwili kujiandaa kufanya kazi yake nje ya tumbo la mama.
Macho ya mtoto anaweza kufumbua na kufumba, pia mtoto anakuwa na uwezo wa kuona mwanga unaomulikwa kwenye tumbo la mama.
Pia uwezo wa mtoto kusikia nao unakuwa umeimarika na anaweza kusikia sauti kutoka nje ya tumbo la mama kama vile mziki au mazungumzo ya watu.
Mama anaweza kumuongelesha au kumuimbia mtoto akiwa tumboni na hiyo inasaidia kujenga mahusiano mazuri kati ya mama na mtoto.
Ubongo wa mtoto nao unaendelea kukua mpaka wisho wa mwezi wa saba mtoto anakuwa ana uwezo wa kutambua sababu ya jambo na madhara yake.
Uwezo wa mtoto kunyonya nao unaimarika katika kipindi hiki na mara nyingi akiwa tumboni ananyonya kidole gumba.
Mifupa ya mtoto nayo inaendelea kukomaa, mateke na ngumi zake tumboni sasa mama anaweza kuzihisi kwa ukubwa wake.
Mapafu ya mtoto yanakuwa yamekamilika kwa kiasi kikubwa na anaweza kushikwa na kwikwi au kikohozi.
Ikitokea mtoto amezaliwa kwenye mwezi huu wa saba anahesabika kuwa mtoto njinti na anaweza kuendelea kukua vizuri chini ya uangalizi maalumu wa madaktari.
Uchovu mwingi, maumivu ya nyonga na maumivu chini ya mgogo mara nyingi huwapata wajawazito katika mwezi huu.
Wakati mwingine maumivu hayo huanzia chini ya mgongo na kushuka chini ya miguu.
Kujikanda kwa maji ya moto au maji baridi kunaweza kusaidia kuondoa maumivu hayo.
Wakati mwingine wajawazito huisi mgandamizo wa misuli ya mfuko wa kizazi kama dalili ya uchungu lakini sio endelevu.
Hali hiyo ni ya kawaida kwa mimba ya miezi saba na inaweza kuisha pale ambapo utabadilisha mkao wako.
Unaweza pia kusoma: