Muonekano wa Giza:

Msaada

Picha inaonesha kielelezo cha mtoto aliyeko tumboni huku kitovu chake kikiwa kimemzunguka shingoni.

Kitovu kinachomfunga mtoto akiwa tumboni

Kitovu kujifunga shingoni kwa mtoto ni moja kati ya hali ya kawaida kutokea wakati wa kujifungua.
Kwa mujibu wa takwimu kati ya watoto 4 wanaozaliwa mtoto mmoja anaweza kuzaliwa kitovu kimejifunga shingoni.
Mara nyingi kitovu kinakuwa hakijamkaba sana mtoto ila kwa mara chache sana inatokea kitovu kinakaba sana shingoni kwa mtoto.
Pia mara nyingi hali hiyo imeripotiwa kutokea pasipo kuwa na madhara kwa mtoto na ni mara chache sana hali hiyo inaweza kusababisha madhara makubwa kwa mtoto.
Pia tafiti zimeonesha kuwa kadri mtoto anavyozidi kukaa tumboni kwa muda mrefu inaongeza uwezekano wa kitovu kumfunga shingo mtoto.
Pia watoto wa kiume wameonekana wana uwezekano mkubwa wa kupata hali hiyo kuliko watoto wa kike.

Hakuna dalili yoyote kwa mama mjamzito ambayo inaashiria kuwa kitovu kimemfunga mtoto shingoni.
Kama kitovu kimemfunga mtoto inaweza kugundulika kama mama atafanya kipimo cha ultrasound kipindi cha ujauzito ila mara nyingi hali hiyo uonekana wakati wa kujifungua.
Na inapotokea katika kipimo imegundulika kitovu kimemfunga mtoto kabla ya muda wa kujifungua haina haja ya kuwa na wasiwasi kwasababu kuna uwezekano wa kujifungua chenyewe kabla ya kwenda leba.
Pia hata wakati wa kujifungua wataalamu wa afya lazima wawai kukilegeza au kukitoa kitovu shingoni kwa mtoto kabla hajaanza kupumua.
Hata hivyo kitovu cha mtoto kina utelezi hivyo inakuwa ngumu sana kujifunga na kukaza sana shingoni kwa mtoto.
Pia hakikisha unamuuliza daktari maswali yako yote kuhusiana na hali hiyo ili kupata uhakika wa usalama wa mwanao na kuondoa wasiwasi wako kama hali hiyo imegundulika kabla ya kwenda leba.

Je nini kinasababisha kitovu kumfunga mtoto akiwa tumboni?
Sababu kubwa ya mtoto kufungwa na kitovu shingoni ni sarakasi zake akiwa tumboni.
Mtoto anayebenuka sana akiwa tumboni ana uwezekano kubwa wa kufungwa na kitovu shingoni.
Pia kuna sababu nyingine zinazoweza kuchangia kitovu kujifunga shingoni kwa mtoto akiwa tumboni.
Kama una mimba ya mapacha kuna uwezekano mkubwa wa kitovu kujifunga kwa mtoto akiwa tumboni.
Kama kuna maji mengi kwenye chupa ya uzazi inaweza pia kusababisha hali hiyo.
Kitovu kirefu cha mtoto kinaongeza uwezekano wa kujifunga shingoni kwa mtoto akiwa tumboni.
Pia kama muundo wa kitovu cha mtoto sio mzuri inachangia kujizungusha kwenye shingo ya mtoto.

Hakuna namna yoyote ya kufanya ili kuzuia kitovu kisijifunge shingoni kwa mtoto na wala kijifunga kitovu kwa mtoto hakuna mahusiano na jambo lolote ambalo mama amelifanya kipindi cha ujauzito.

0
0
1