Muonekano wa Giza:

Msaada

Pichani anaonekana mwanamke akiwa mikono yake yote miwili ameshikilia chini ya tumbo lake huku taiti yake ikionekana imeloana kati kati ya mapaja.

Hali ya Uke kuvuta wakati wa kukojoa ukiwa Mjamzito

Ukiwa Mjamzito kuna mabadiliko mengi hutokea mwilini tofauti na hali yako ya kawaida uliyoizoea.
Kuna mabadiliko ya kawaida kwa mjamzito na kuna mengine si ya kawaida kwa mjamzito.

Ni muhimu kuwa na taarifa kuhusu mabadiliko mbalimbali yanaweza kutoke katika kipindi chote cha ujauzito ili kuweza kutambua hali ambayo si ya kawaida ili kutafuta msaada unaohitajika.

Hapo chini ni makala ambazo zimeelezea hali zinavyokuwa kwa Mimba ya mwezi mmoja mpka miezi nane.

Mimba ya Mwezi Mmoja inakuaje?

Mimba ya Miezi Miwili inakuaje?

Mimba ya Miezi Mitatu inakuaje?

Mimba ya Miezi Minne inakuaje?

Mimba ya Miezi Mitano inakuaje?

Mimba ya Miezi Sita inakuaje?

Mimba ya Miezi Saba inakuaje?

Mimba ya Miezi Nane inakuaje?

Uke kuvuta unapoenda kukojoa ukiwa na Mimba!

Moja ya hali inayowapata wajawazito ni kuhisi uke unavuta wakati wa kukojoa.
Hali hii ni ya kawaida kutokea wakati wa ujauzito, kama imewahi kukutokea huna haja ya kuwa na wasisi.

Hali ya uke kuvuta unapoenda kukojoa ukiwa na Mimba inaweza kutokea kwasababu zifuatazo:

Kadri mtoto anavyozidi kukua mfuko wa kizazi nao hukua na kuongezeka uzito.
Uzito wa mtoto kwenye mfuko wa kizazi husababisha kibofu cha mkojo kujiminya.

Kibofu cha mkojo kikiminywa hupunguza uwezo wa kutunza mkojo mwingi wa muda mrefu hivyo husababisha hali ya kukojoa mara kwa mara kwa mama mjamzito.

Kibifu cha mkojo kinapokuwa kimejaa huminya mfuko wa kizazi na unapoenda kukojoa baada ya mkojo kutoka kwa ghafla huishitua misuli ya mfuko wa kizazi.

Misuli hiyo inaposhituliwa husababisha hali ya kubana na kuachia hali ambayo husababisha mjamzito kuhisi uke unavuta akiwa anakojoa.

Kuna hali nyingine pia kwa uchache zinaweza kusababisha hali hii kwa mjamzito:

Kama hunywi maji kwa wingi:
Mkojo ambao umekolea sana kwa upungufu wa maji huishitua misuli ya kibofu kujiminya ghafla wakati wa kukoja.
Hali hiyo inaweza kuambukizwa kwa misuli ya mfuko wa kizazi na kusababisha hali ya uke kujivuta.
Hivyo mara zote unashauriwa kuhakikisha unakunywa maji kwa wingi katika kipindi cha ujauzito.

Mkojo Mchafu (UTI):
Maambukizi ya Bakteria kwenye njia ya Mkojo (UTI) inaweza kusababisha hali ya kuvuta kwa uke wakati wa kukojoa ukiwa ni mjamzito.
Ukiwa na tatizo hili huambatana na dalili nyingine kama vile kuhisi kwenye haja ndogo mara kwa mara na ukifika chooni unatoa vitone kidogo tu vya mkojo.
Pia mkojo wako unaweza kuonekana una rangi ya maziwa au una rangi ya mkojo iliyokolea sana na mkojo unaweza kuwa unatoa harufu isiyo ya kawaida.
Kwa baadhi ya wanawake wanaweza kuona vitone vya damu kwenye mkojo.
Tatizo hili linapokaa kwa muda mrefu bila matibabu linaweza kusababisha homa na kusababisha mambukizi kwenye Figo.

Kama ni mjamzito na unapata hali ya kuvuta uke ukiwa unakojoa, pia hali hiyo ikiwa inaambata na dalili hizo za Mkojo Mchafu (UTI) ni muhimu kumuona Daktari kwa uchunguzi zaidi.

1
0
1