Mimba ya miezi sita inakuaje?
Shauku ya wajawazito wengi ni kutaka kujua maendeleo ya mimba toka siku anajigundua kuwa ni mjamzito mpaka siku ya kujifungua.
Ili kufahamu hayo yote kuhusu maendeleo ya mimba kwanzia mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa tisa, fuatilia tovuti yetu kufahamu zaidi.
Katika makala hii tufahamu kuhusu mimba ya miezi sita inakuaje.
Kama una mimba ya miezi sita tarajia mambo haya yafuatayo:
Kupata choo kigumu:
Hii ni kwasababu ya mgandamizo wa mfuko wa kizazi kwenye utumbo.
Maumivu sehemu mbalimbali hasa maumivu ya mgongo, maumivu ya nyonga na maumivu chini ya kitovu:
Miwasho:
Hasa miwasho ya tumbo ni kutokana na kutanuka kwa ngozi ya tumbo.
Kizunguzungu:
Ni kutokana na damu nyingi kuelekea kwenye kazazi kuliko kwenye ubongo.
Kuvimba miguu na maumivu ya misuli kwenye miguu:
Njaa kuuma:
Ni kutokana na mahitaji ya virutubisho vya mtoto kuongezeka na mtoto kuendelea kukua.
Pia unaweza kuendelea kupata kiungulia:
Kuwa na hamu na uchaguzi wa vyakula mbalimbali:
Pia harufu:
Pia matiti yanaendelea kuongezeka ukubwa:
Tumbo linakuwa kubwa kiasi cha kukufanya uanze kuvaa mavazi ya mjamzito.
Kitovu pia kinaanza kutokeza nje kwa baadhi.
Dalili hizo ni za kawaida kwa wajawazito na huisha mara baada ya kujifungua na zingine huisha tu baada ya siku kadhaa ila kama
zitakufanya kuwa na hali mbaya sana ni vizuri kumuona daktari kwa msaada zaidi.
Pia kuwahi au kuchelea kuziona dalili hizi kabla au baada ya miezi husika isikupe presha kwasababu mimba huja tofauti kwa
kila mtu na dalili hizi haziwezi kuwa sawa kwa kila mtu au kwa kila ujauzito wako.
Maendeleo ya mtoto tumboni kwa mimba ya miezi sita anakuwa amekua mpaka kufikia urefu wa inchi 7 mpaka inchi 12.
Mtoto anakuwa amekamilika ukuaji wake kwa kiasi kikubwa, na anakuwa na uwezo wa kusikia sauti zinazotoka nje ya tumbo, kuwa na makini na uchokiongea.
Unaweza pia kusoma: