Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

picha hii imeonesha mama akiwa anambusu mtoto wake wenye umri wa miezi miwili

Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi miwili (2)

Baada ya kujifungua shauku ya wazazi ni kujua, kuona maendeleo na ukuaji mzuri wa mtoto.

Katika makala hii tufahamu kuhusu ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi miwili.

Kwa miezi miwili mtoto hukua kwa kasi kulinganisha na mwezi mmoja uliopita.

Misuli ya mtoto inaendelea kuimarika, miguu na mikono yake anaweza kuichezesha na kujinyoosha kumfanya aonekane mrefu.

Watoto wa miezi miwili wanaanza kutambua mikono na vidole vyao, wanaweza kushikilia vitu pia wanaweza kujishika mikono yao wenyewe.

Wanaanza kujifunza kudhibiti matendo yao na wanarusharusha mateke kwa nguvu.

Shingo ya mtoto inaendelea kukaza kama mtoto atalalia tumbo anaweza kunyanyua kichwa na kuzungusha kichwa kuangalia upande na baadhi ya watoto wanakuwa na uwezo wa kunyanyua kifua pia.

Kwa baadhi ya watoto wa miezi miwili japo kwa uchache wanaanza kulala usiku kucha hata kama hujapata bahati hiyo kwa muda huo ila kuna muda lazima mtoto atapata usingizi kwa muda mrefu zaidi.

Mtoto anaanza kutambua sura ya mzazi na anakuwa anakuangalia ukiwa unazungumza nae.
Na mtoto anakuwa anafurahia kuangalia sura yako na kutabasamu akikuangalia.

Kwa watoto wa miezi miwili wana uwezo wa kufuatisha vitu kwa macho na wanapenda kuangalia vitu vyenye rangirangi.

Mtoto anaanza kutoa sauti na miguno, anatoa sauti kama vile ‘a’ au ‘o’.

Ili kumsaidia mwanao kukua vizuri na maendeleo yake kuwa mazuri:

Jitahidi kutumia muda mwingi na mwanao kumsomea, kumuimbia na kumuongelesha itamsaidia kuanza kujifunza sauti na maneno.

Cheza na mwanao na muache achezee vitu tofautitofauti vyenye maumbo na rangi mbalimbali.

Watoto wanapenda kukutazama usoni, jitahidi kutabasamu kwa mtoto inamsaidia kujihisi yuko salama zaidi.

Kumlazia mtoto tumbo angalau kwa dakika 1 mpaka 5 inamsaidia kukaza misuli ya shingo na mwili ambayo itamsaidia kukaa na kutambaa baadae.
Ila Muda wote hakikisha unamlazia mtoto mgongo.

Ukuaji wa watoto hutofautiana sana, kuna watoto wanaweza kuwahi na kuna wengine wanachelewa.
Kwa watoto wa miezi miwili ukiona mambo haya unashauriwa kumuona daktari.

Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi mitatu (3)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa mwezi mmoja (1)

0
0