Muonekano wa Giza:

Msaada

Kwenye picha kumeonesha mtoto mwenye tatizo la kichwa kikubwa akiwa amelala kitandani.

Tatizo la kichwa kikubwa kwa watoto (Sababu, Dalili na Tiba)

Tatizo la kichwa kikubwa kwa watoto husababishwa na maji kujaa kwenye ubongo.

Maji hayo huzalishwa kawaida kwenye ubongo na kuzunguka kwenye ubongo ili kusafisha na kuupa virutubisho ubongo.
Pia maji hayo husaidia kuukinga ubongo dhidi ya mitikisiko inayoweza kutokea kwenye kichwa.
Kwa kawaida maji hayo huzalishwa kwenye ubongo na kutolewa nje ya ubongo kupitia mishipa ya damu kwenye ubongo.

Kuna kiwango maalumu kinachohitajika kwenye ubongo kinachozidi hutolewa nje kupitia mishipa ya damu.
Maji hayo yanaweza kuzidi kwenye ubongo endapo itatokea hitilafu kwenye uzalishaji au utoaji wa maji ya ziada kwenye ubongo.

Tatizo hili linaweza kumpata mtu yoyote ila wenye uwezekano mkubwa wa kupata tatizo hili ni watoto wachanga na wazee wa miaka 60 au zaidi.

Maji yanapojaa kwenye ubongo husababishwa kichwa kuwa kikubwa kuliko kawaida kwa watoto wachanga kwasababu mifupa ya fuvu la kichwa inakuwa bado haijafunga vizuri.

Kwa watu wazima wanaopata tatizo la maji kujaa kwenye ubongo haiwezi kusababisha kichwa kuwa kikubwa ila hupata hupata madhara ndani ya ubongo.

Unaweza kuona dalili hizi zifuatazo kwa mtoto ambaye ubongo umejaa maji, na ni muhimu kumuwaisha hospitali kupata matibabu ya haraka itasaidia kumuepusha na kuwa na kichwa kikubwa.

Dalili hizo ni:

Unapoona dalili hizo kwa mtoto ni muhimu kuwahi hospitali, tatizo hilo likitibiwa mapema kabla ya kusababisha madhara makubwa kwa mtoto ni vizuri.

Mtoto mchanga kuzaliwa na tatizo la maji kujaa kwenye ubongo inaweza kusababishwa na,

0
0
1