Muonekano wa Giza:

Msaada

Pichani kuna mwanamke mjamzito akiwa amezungusha mikono yake yote miwili tumboni kwake, pia tumbo lake lina mstari mweusi uliokolea katikati ya tumbo lake.

Mstari mweusi kwenye tumbo la mjamzito

Japo si kwa wajawazito wote ila kwa wajawazito wengi karibia asilimia 80 huwa na mstari mweusi unaokatiza kutoka kwenye kinena mpaka kwenye kitovu.
Mstari huu unakuwepo kwa wanawake wengi hata kabla ya kuwa mjamzito ila rangi yake inakuwa haijakolea sana kiasi ambacho sio rahisi kuuona.
Mstari huo hukolea na kuonekana vizuri kwenye tumbo la mjamzito hasa baada ya wiki 20 za ujauzito.
Mstari huo hupotea wenyewe na kurudi kama uliyokuwa baada ya kujifungua.
Inaweza kuchukua wiki kadhaa mpaka miezi mstari huo kupotea kurudi kama uliyokuwa awali.

Pia inatokea kwa baadhi ya wanawake mstari huo hubakia tuboni au unachelewa sana kupotea kurudi kama awali.
Mpaka sasa hakuna mtu ambaye amefanikiwa kujua nini hasa kazi ya mstari huo tumboni kwa mjamzito.
Ila baadhi ya wataalau walijaribu kuelezea kuwa mstari huo humsaidia mtoto mtoto kulitafuta ziwa wakati wa kunyonya.

Je kitu gani kinasababisha mstari wa mimba kwa mjamzito?
Mstari wa mimba ni mstari wa asili unaotokea wenyewe kwasababu ya ongezeko la homoni mbalimbali ndani ya mwili wa mjamzito.
Sababu ya moja kwa moja inayosababisha mstari wa mimba bado haijulikani ila baadhi ya wataalamu wanasema mstari huo husababishwa na seli za ngozi zinazozalisha weusi kwenye ngozi kuongezeke eneo hilo la tumbo.
Seli hizo hizo pia huongezeka kwenye eneo linalozunguka chuchu kwenye matiti na kusababisha kuongezeka kwa weusi kwenye chuchu wakati wa ujauzito.

Je inawezekana kuufanya mstari wa mimba usionekane wakati wa ujauzito?
Jibu ni hapana, hakuna namna ambayo unaweza kufanya kuufuta mstari wa mimba usionekane wakati wa ujauzito.
Na wataalamu hawashauri kutumia vipodozi vya aina yoyote ile au krimu za kujichubua kupaka tuboni wakati wa ujauzito ili kujaribu kuufuta stari huo.
Unaweza kutumia krim za kujichubua mara baada ya kujifungua na ukiwa haunyonyeshi kama mstari huo utakuwa kero kwako.
Pia unaweza kutumia makeup kufunika mstari huo kama utakuwa kero au kama unachukua muda mrefu kupotea mara baada ya kujifungua.
Na sio tu wajawazito ndio lazima wawe na mstari wa mimba bali kuna baadhi ya wanawake ambao si wajawazito pia hata watoto mstari huo uonekana mweusi tumboni kama mstari wa mimba.
Hiyo husababishwa na mabadiliko ya homoni mwilini, pia kuna madawa na baadhi ya matatizo ya kiafya husababisha mstari huo kuwa kama mstari wa mimba hata kama huna mimba.
Ukiona hali hiyo ni vizuri kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi wa afya yako.

0
0
1