Muonekano wa Giza:

Msaada

Picha inamuonesha mama mjamzito picha ya kielelezo cha jinsi ambavyo mtoto anakaa tumboni kwa mama mama mwenye mimba ya miezi kumi

Ukuaji wa mtoto tumboni kwa mama mjamzito mwenye mimba ya miezi kumi.

Mimba ni mchakato wa asili wa muda mrefu kwa binadamu, inachukua takribani siku 280 au wiki 40 ambayo pia inakadiriwa miezi 9 mpaka mtoto kuzaliwa na kuwa na uwezo wa kuyaishi mazingira ya nje ya tumbo la mama.

Mchakato huu kwa mtoto huanzia kwenye seli moja tu ambayo ni mchanganyiko wa yai la mama na mbegu ya baba.
Seli hiyo hugawanyika mpaka kupata mamilioni mengine ya seli ambazo huunda viungo mbalimbali ndani na nje ya mwili wa mtoto.

Kuna hatua mbalimbali ambazo mtoto tumboni anazipitia kutoka yai la mama kurutubishwa mpka wakati wa kujifungua.
Tufahamu nini kinachoendelea tumboni kwa mama mjamzito katika miezi yake yote 9 mpaka kujifungua.

Mwezi huu wa kumi ambao ni kati ya wiki 37 mpaka wiki 40 za ujauzito.
Wiki za mwisho kabisa kwenye ujauzito kuelelekea kujifungua.

Katika mwezi huu mtoto huanza kubadilisha mkao wake kujiandaa kutoka nje ya tumbo.
Kwa asilimia kubwa mtoto tumboni hujigeuza kichwa kuelekea chini kwenye nyonga ya mama.

Ni kipindi ambacho mama mjamzito hupitia hali ngumu kidogo kwasababu ya mtoto kujigeuza ndani ya tumbo.
Na mama anaweza kuanza kuhisi jinsi mtoto anavyoshuka kwenye nyonga.

Mtoto huongezeka uzito kwa kasi kila wiki mpaka kufikia kilo zake za kuzaliwa nazo.
Kwa kawaida urefu wa mtoto unaweza kufikia inchi 18 mpaka 20.
Na uzito wake unaweza kufikia wastani wa kilo 3 mpaka 4.

Kwa mama mjamzito kipindi hiki ndicho cha kujiandaa kwani uchungu unaweza kutokea siku yoyote kwenye wiki hizi za mwisho.

Hizo ni baadhi ya dalili ambazo mjamzito anaweza kuzipata katika wiki hizi za mwisho kama ishara ya kuwa muda wa kujifungua umefika.

0
0
1