Jinsi ya kutunza kitovu cha mtoto mchanga mpaka kikatike
Wakati wa ujauzito mtoto tumboni hupokea virutubisho, hewa safi na mahitaji yake mengine kutoka kwa mama kupitia kondo la uzazi na kitovu.
Baada ya kuzaliwa kondo na kitovu havina kazi tena hukatwa kumtenganisha mtoto na kondo.
Kipande kidogo cha kitovu kilichobanwa hubaki kikining’inia kwa mtoto.
Kipande hicho baada ya muda hukauka na kudodondoka chini chenyewe.
Kwa kawaida kitovu cha mtoto mchanga kinakatika chenyewe baada ya wiki moja mpaka tatu baada ya kuzaliwa.
Katika makala hii ningependa tufahamu mambo mbalimbali ambayo yanashauriwa na wataalamu jinsi ya kulinda na kutunza kitovu cha mtoto mpaka kitakapo katika.
Katika kipindi hicho kifupi mpaka kitovu kitakapokauka hakikisha:
1. Kitovu kinakuwa kikavu muda wote:
Kama unamvalisha mtoto nepi au pampas hakikisha unaikunja kwa mbele ili isifunike kitovu kama bado hakijakatika.
Ni muhimu kukiacha kitovu kipulizwe na upepo ili kikauke haraka.
2. Muogeshe mtoto kwa kumfuta na kitambaa.
Kumuogesha mtoto mchanga kwa kumfuta na kitambaa inashauriwa kwasababu inasaidia kukinga kitovu kisiloane na maji ili kikauke mapema.
3. Kiache kitovu kikatike chenyewe usikikate.
Hata kama sehemu ya kitovu imebakia kidogo ili kikatike usishawishike kukivuta kitovu ili kukikata kiache paka kitakapokatika chenyewe.
Na utakapoona dalili zozote kati ya hizi kwenye kitovu cha mtoto ni muhimu kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.
- Kama utaona usaa unadodoka kutoka kwenye kitovu.
- Kama utaona ngozi ya kwenye kitovu imekuwa nyekundu au imeviba.
- Pia kama kitovu cha mtoto kitakuwa hakijakatika baada ya wiki 3 toka kuzaliwa muone daktari kwa uchunguzi zaidi.
Unaweza pia kusoma: