Mtoto aliyetanguliza makalio wakati wa kujifungua
Kwa kawaida mtoto hutanguliza kichwa wakati wa kujifungua.
Kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha mtoto kutokutanguliza kichwa wakati wa kujifungua.
Katika video hii tufahamu sababu ambazo zinaweza kusababisha mtoto kutanguliza makalio wakati wa kujifungua.
Matatizo ya kuzaliwa nayo mama:
Mama anaweza kuwa amezaliwa na ulemavu kwenye mfuko wa uzazi kama vile, kuwa na mifuko miwili ya uzazi au mfuko wa uzazi uliotenganishwa katikati.
Hali hiyo huchangia kwa kiasi kikubwa mtoto kushindwa kujigeuza wakati wa kujifungua.
Kondo kujishikiza chini ya fuko wa kizazi au kuziba shingo ya kizazi:
Sababu nyingine inayochangia kwa kiasi kikubwa mtoto kushindwa kujigeza tumboni ni kondo kujishikiza chini ya mfuko wa kizazi.
Kushindwa kujigeuza mtoto mtumboni husababisha kuzaliwa akiwa ametanguliza makalio.
Uvimbe kwenye mfuko wa kizazi:
Pia kwa mjamzito ambaye ana tatizo la uvimbe kwenye mfuko wa kizazi, uvimbe huo unaweza kusababisha mtoto kushindwa kujigeuza
tumboni na kuzaliwa akiwa ametanguliza makalio wakati wa kujifungua.
Kujifungua kabla ya muda:
Mjamzito ambaye amejifungua kabla ya wiki 32 za ujauzito kuna uwezekano mkubwa wa mtoto kutanguliza makalio kwasababu mtoto
huanza kujigeuza kuelekeza kichwa chini baada ya wiki 32 za ujauzito.
Ulemavu wa misuli au ulemau mwingine kwa mtoto:
Kama mtoto ana ulemavu wa misuli wa kuzaliwa nao inaweza kusababisha mtoto kukosa nguvu ya kujigeuza akiwa tuboni.
Unaweza pia kusoma: