
Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa mwezi mmoja (1)
Baada ya kujifungua shauku ya wazazi ni kujua kuona maendeleo na ukuaji mzuri wa mtoto.
Katika makala hii tufahamu kuhusu ukuaji na maendeleo ya mtoto wa mwezi mmoja.
Kwa mwezi mmoja wa ukuaji wa mtoto baada ya kuzaliwa kuwa nae karibu, kuhakikisha amekula au amenyonga vizuri na kulala vizuri ni vitu vya muhimu kwa ukuaji wa mtoto.
Mtoto anawaza kuwa analia sana kipindi hiki, sababu zinaweza kuwa njaa au nepi imeloana pia wakati mwingine mtoto anaweza kulia tu bila sababu inayoeleweka zingatia kuwa ilo ni jambo la muda tu litapita.
Kwa kawaida mtoto napozaliwa wiki ya kwanza hupoteza wastani wa asilimia 10 ya uzito wake na baada ya wiki 2 uzito wake unarudi kawaida na kuendelea kukua kawaida.
Kwa mwezi mmoja, watoto wengi matendo yao yanakuwa si ya hiyari. Wanakuwa na uwezo wa kunyonya, kumeza, kutafuta maziwa na kushika vitu ambavyo vinawekwa kwenye viganja vyao ila mara nyingi wanakuwa wamekunja ngumi.
Wanakuwa na uwezo wa kusogeza mguu mmoja mbele kama migiuu itasimamishwa sehemu iliyonyooka.
Kama mtoto atataka kuanguka kwa nyuma wanashituka kwa kunyanyua miguu na mikono, huchezesha macho na kupumua harakaharaka.
Mpaka mwishoni mwa mwezi wa kwanza watoto wengi wanakuwa na uwezo wa kunyanyua kichwa na kugeuza kichwa upande kama utamlazia tumbo na misuli ya shingo inaendelea kukomaa zaidi siku zijazo.
Kwa mwezi mmoja watoto wengi wanaanza kuangalia na kufuatilia vitu kwa macho yao.
Kama utamsogelea kwa karibu sana usoni atakuangalia machoni kwa muda mrefu na watoto wengi huanza kuzitambua sura za wazazi wao wakiwa na mwezi mmoja.
Watoto wa mwezi mmoja wanapenda kusikiliza sauti yako pia wanashitushwa na sauti kali ya makelele.
Ili kumsaidia mtoto wako kukua vizuri:
Pata muda wa kukaa na mwanao, kuangaliana macho kwa macho na kutabasamu kwa mtoto kunamsaidia kujenga mahusiano mazuri na kujihisi yuko salama.
Imba na soma kwa sauti mbele ya mwanao hata kama haelewei chochote ila anafurahia kusikia sauti yako.
Kucheza na mwanao pia inasaidia kuimarisha mahusiano yenu.
Kwa kumsaidia mwanao kukaza misuli yake ya shingo inashauriwa kumlazia mtoto tumbo angalau dakika 1 mpaka 5 na uwepo karibu kumuangalia.
Ukuaji na maendeleo ya watoto hutofautiana sana mwanao anaweza kuwahi au kuchelewa kuonesha hatua hizi za ukuaji.
Itakubidi kumuona daktari kwa msaada zaidi ikiwa utaona dalili hizi kwa mwanao:
- Mtoto hanyonyi au hali vizuri.
- Mara kwa mara analala sana zaidi ya masaa 16 kwa siku.
- Kama mtoto anashindwa kuchezesha mikono na miguu yake.
- Kama mtoto hawezi kuifuatisha sura yako kwa macho yake au anashindwa kufanya ishara yoyote anapokuaona.
- Kama mtoto anaonekana kama hasikii chochote na hashituki hata kama kuna makelele.
- Na kama una wasiwasi kuhusu uliaji au ulalaji wa mtoto wako.
Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi miwili (2)
Unaweza pia kusoma: