
Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi mitatu (3)
Baada ya kujifungua shauku ya wazazi ni kujua kuona maendeleo na ukuaji mzuri wa mtoto.
Katika makala hii tufahamu kuhusu ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi mitatu.
Kwa miezi mitatu mtoto wako anakuwa ameshakujua tarajia kuona akitabasamu mara kwa mara anapokuona na kuongea na wewe kwa namna yake anayoijua mwenyewe.
Vilio vya mara kwa mara vinaweza kuwa vimepungua kwa mtoto.
Kwa watoto wengi wa miezi mitatu wanakuwa wameacha kusumbua sana usiku, wanaweza kulala usiku kucha yani kwa masaa 5 au 6 kwa usiku.
Kwasababu watoto wanakuwa tofauti hauna haja ya kuwa na wasiwasi kama mwanao hapati usingizi kwa masaa hayo usiku.
Kwa mtoto wa miezi mitatu sehemu laini nyuma ya kichwa chake inakuwa imefunga inabakia sehemu ya utosi pekee.
Kwa miezi mitatu ya ukuaji wa mtoto, misuli ya mikono inakuwa imara wanaanza kujaribu kushika vitu wanavyoviona na kuvipeleka mdomoni.
Vile vile wanakuwa na uwezo wa kujishika mikono yao.
Misuli ya shingo inakuwa imekaza na anakuwa na uwezo wa kuzungusha kichwa na anakuwa na uwezo wa kunyanyua kichwa chake ukimkalisha.
Kama utamlazia tumbo unaweza kuona anajigeuza kulalia mgongo, anaweza kunyanyua kichwa au anaweza kunyanyua kifua chake kwa mikono.
Wanakuwa na uwezo wa kurusharusha mikono na kurusha mateke kwa nguvu na kama utajaribu kumsimaisha anakaza miguu yake akijaribu kusimama.
Kwa mtoto wa miezi mitatu japokuwa hana uwezo mzuri wa kudhibiti matendo yake kati ya mikono na macho ila anaweza kuviangalia vitu vinavyomvutia na kuvigusa au kuvitikisa.
Watoto wa umri huu wanaweza kuwa wanatabasamu tu hata kwa watu wasiowajua ila kwa kawaida wanawafahamu wazazi wao vizuri.
Ubongo wa mtoto pia unakua kwa kasi na anakuwa na uwezo wa kuwatambua watu kwa kuwaona, harufu, na sauti zao.
Kwa miezi mitatu watoto wanaanza kutambua hisia mbalimbali na njia za mawasiliano pia anaijua sauti yako na anaweza kukugeukia pindi anaposikia sauti yako.
Watoto wanaweza kuwa wanaanza kucheka kwa sauti pia wanatoa sauti kama mtu anayepuliza maji mdomoni na anajaribu kukujibu kama utakuwa unamuongelesha.
Ili kumsaidia mtoto kukua vizuri na kuwa na maendeleo mazuri:
Katika kipindi hiki mtoto anaanza kujifunza lugha, jitahidi kuongea au kumsomea mwanao vitabu mara kwa mara kadri unavyoweza.
Unaweza kumsaidia mwanao kukomaa misuli ya shingo na mgongo kwa kumuwekea matoy mbele yake wakati amelalia tumbo.
Unaweza kumgusa mtoto na vitu mbalimbali kama vile mayoya au tishu ili kuchamsha hisia zake za mguso.
Ukuaji wa watoto hutofautiana sana, kuna watoto wanaweza kuwahi na kuna wengine wanachelewa. Kwa watoto wa miezi mitatu ukiona mambo haya unashauriwa kumuona daktari kwa msaada zaidi.
- Kama mtoto anashindwa kutabasamu na ana zaidi ya wiki 8.
- Anashindwa kunyamaza hata kwa muda kidogo wakati umemchukua kumbembeleza.
- Upande mmoja wa mwili wake unaonekana kuwa na nguvu kuliko upande mwingine.
- Kama mtoto anaendelea kukaza ngumi anashindwa kufungua viganja viganja vyake.
- Mtoto hashituki hata kwenye makele ya gafla.
- Na kama mtoto hanyonyi vizuri.
Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi minne (4)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi miwili (2)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa mwezi mmoja (1)
Unaweza pia kusoma: