
Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi minne (4)
Baada ya kujifungua shauku ya wazazi ni kujua au kuona maendeleo na ukuaji mzuri wa mtoto.
Katika makala hii tufahamu kuhusu ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi minne.
Kuanzia miezi minne watoto wanaanza kujifunza kudhibiti matendo yao, wanaanza kutambua wanachokifanya, wanachokiona, wanachokishika na wanachokisikia na usumbufu wao wa kuchezacheza unaanza kuongezeka.
Mifupa ya mtoto inakua kwa haraka na kuongezeka urefu.
Watoto wa miezi minne wanaanza kujifuza mengi kuhusu mazingira yao yanayowazunguka.
Kwa watoto wa miezi mine pia wanaanza kuonesha kutamani vyakula vingine tofauti na kunyonya na anaanza kujifunza kutafuna.
Watoto wanakuwa na uwezo wa kushika vitu na kujaribu kupeleka mkono mdomoni.
Hii ni hatua ya kawaida kwa mtoto kwasababu naanza kujifunza na kuwa tayari kula vyakula vingine tofauti na kunyonya.
Jitahidi kuwa makini na vitu vinavyokuwa karibu yake visiwe vidogo vinavyoweza kuingia mdomoni na kumsababishia madhara.
Uwezo wa mtoto kuona unakua umeongezeka na anakuwa na uwezo wa kuhusianisha kati ya vitu anavyoviona na anavyovinusa, anavyovisikia na navyovishika.
Kwa miezi minne mtoto anakuwa amechangamka na unaweza mkaangaliana, ukaongea nae, mkacheka na kutabasau kwa pamoja.
Pia watoto wanapenda kujiangalia kwenye kioo na anaweza kutabasau na kuongea na taswira yake.
Kwa umri huu mtoto anaweza kuonesha hisia zake kama akiwa na hasira na akiwa amechoka au muda mwingine analalamika tu bila kulia.
Unaweza kutambua ni muda gani mwanao analia akiwa na njaa au kama amechoka.
Ili kumsaidia mwanao kukua na kuwa na maendeleo mazuri jitahidi kufanya mambo yafuatayo:
Endelea kuongea na mwanao au kumsomea vitabu inamsaidia kujifunza lugha.
Mtoto anapenda kukuona ukiimba , ukimsomea kitabu, ukichezea matoy na anapenda kukusikiliza ukitoa sauti mbalimbali zinazomfurahisha.
Kwa kawaida watoto wana hatua zao za ukuaji tofauti kuna wengine wanachelewa na kuna wengine wanawahi kuonesha hatua hizi.
Kwa watoto wa miezi mine unapoona dalili hizi ni muhimu kuwahi hospitali kwa msaada zaidi.
- Kama mtoto haoneshi kuvutiwa na vitu vinavyomzunguka.
- Kama mtoto anaonekana kama hakujui.
- Kama mtoto hatoa sauti yoyote.
- Kama mtoto hawezi kufungua vidole vyake kufungua ngumi.
- Kama mtoto hawezi kurusha mateke na miguu yake muda wote ameikunja.
- Kama mtoto hana uwezo wa kufuatisha vitu kwa macho, au anashindwa kukuangalia usoni.
- Kama mtoto anashinwa kugeuka akisikia sauti yako hao haonekani kushituka hata kama akisikia makelele ya ghafla.
- Na mwisho ni Kama mtoto anaonekana kutokuwa na furaha au kutokutulia mara kwa mara.
Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi mitano (5)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi mitatu (3)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi miwili (2)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa mwezi mmoja (1)
Unaweza pia kusoma: