Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi mitano (5)
Baada ya kujifungua shauku ya wazazi ni kujua au kuona maendeleo na ukuaji mzuri wa mtoto.
Katika makala hii tufahamu kuhusu ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi mitano.
Kwa watoto wa miezi mitano ukuaji na maendeleo yao ni ya haraka kuliko miezi ya nyuma.
Wanajifunza mengi kuhusu mazingira yanayowazunguka na namna gani wanaweza kuishi nayo.
Ni jambo la muhimu kuanza kuandaa mazingira salama kwa mwanao nyumbani kwasababu muda wowote anaweza kuanza kujisogeza na anaweza kuanguka.
Kwa mtoto wa miezi mitano tarajia kumuona muda wowote anaanza kukaa chini bila sapoti ya kumshikilia.
Ila kaa karibu nae au muwekee vitu vilaini pembeni ili hata kama ataanguka asiumie.
Kama atalalia tumbo anakuwa na uwezo wa kunyoosha miguu na mikono yake na kujipinda mgongo kuangalia juu.
Kama atakuwa amelalia mgongo anakuwa na uwezo wa kuinua kichwa na mageba.
Pia kwa watoto wa miezi mitano wanaweza kujibinua kulalia mgongo kama alikuwa amelalia tumbo.
Watoto wa miezi mitano wanaendelea kuchunguza kila kitu kwa mdomo kwasabu wanaweza kushika kitu na kukipeleka mdomoni kiurahisi.
Wanakuwa na uwezo wa kupiga vitu na kutikisa vitu wanavyovishika, pia mtoto anaweza kuboreka kama ataachwa peke yake kwa muda mrefu.
Kwa miezi mitano watoto wanaweza kuwa na uwezo wa kukuambia nini wanataka mfano anaweza kunyanyua mikono yake akiwa anataka umbebe au analia ukiwa unaondoka na kumuacha peke yake.
Watoto wanaendelea kujifunza namna ya kuzungumza na kwa kawaida watoto wanakuwa wanapiga makelele kwa kupuliza mate.
Na wanakuwa na uwezo wa kusikiliza na kutambua vyanzo vya sauti mbalimbali.
Ili kumsaidia mtoto kuwa na ukuaji mzuri na maendeleo mazuri:
Ongea nae na msikilize mwanao, tumia hisia na sauti tofautitofauti kujibu sauti ya mtoto inamsaidia kujifunza namna ya kufanya mazungumzo na jinsi ya kuonesha hisia zake.
Cheza na mtoto mara nyingi kadri uwezavyo, kwa kumsomea vitabu, kumuimbia, kumlazia tumbo, kuigiza sauti tofauti za kufurahisha na kumpa matoy ya kuchezea.
Kwa kawaida watoto hukua tofauti, kuna wengine wanawahi na kuna wengine wanachelewa kuonesha hatua hizi za ukuaji.
Usimlinganishe mtoto wako na mtoto mwingine, ila kwa miezi mitano unapoona mambo haya yafuatayo kwa mwanao unashauriwa kumuona daktari kwa msaada zaidi.
- Kama mtoto anaonekana kama hakutambui mzazi wake au haoneshi kuvutiwa kabisa na vitu vinavyomzunguka.
- Kama mtoto hatoi sauti yoyote.
- Kama mtoto hawezi kufungua viganja vyake vya mkono, hawezi kurusha mateke na miguu yake muda wote ameikunja.
- Kama mtoto hana uwezo wa kufuatilia vitu kwa macho na hawezi kukuangalia machoni.
- Kama mtoto hageuki anaposikia sauti yako na kama hashituki hata anaposikia makelele.
- Na mwisho ni Kama mtoto hana furaha na anakuwa hatulii kwa muda mrefu.
Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi sita (6)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi minne (4)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi mitatu (3)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi miwili (2)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa mwezi mmoja (1)
Unaweza pia kusoma: