Mimba ya miezi minne inakuaje?
Shauku ya wajawazito wengi ni kutaka kujua maendeleo ya mimba toka siku anajugundua kuwa ni mjamzito mpaka siku ya kujifungua.
Ili kufahamu hayo yote kuhusu maendeleo ya mimba kwanzia mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa tisa, fuatilia tovuti yetu kufahamu zaidi.
Katika makala hii tufahamu kuhusu mimba ya miezi minne inakuaje.
Kama una mimba ya miezi minne tarajia mambo haya yafuatayo:
Kuwa na maumivu ya mgogo:
Kiungulia:
Kuwa na michirizi hasa tumboni:
Kutanuka kwa mishipa ya damu inayozunguka kitovu:
Kupata shida ya kupumua:
Hii ni kwasababu ya ukuaji wa mfuko wa kizazi unaozuia mapafu kutanuka vizuri.
Pua kuvimba na mafua:
Maumivu ya fizi na fizi kutoa damu:
Kupata choo kigumu:
Maumivu chini ya tumbo kutokana na kutanuka kwa nyonga:
Dalili hizo ni za kawaida kwa wajawazito na huisha mara baada ya kujifungua na zingine huisha tu baada ya siku kadhaa ila kama
zitakufanya kuwa na hali mbaya sana ni vizuri kumuona daktari kwa msaada zaidi.
Pia kuwahi au kuchelea kuziona dalili hizi kabla au baada ya miezi husika isikupe presha kwasababu mimba huja tofauti kwa
kila mtu na dalili hizi haziwezi kuwa sawa kwa kila mtu au kwa kila ujauzito wako.
Kwa mimba ya miezi minne unaweza kuanza kuhisi mtoto anacheza tumboni, hii itategemeana na baadhi ya mambo kama vile
mahali kondo lako limejishikiza, kama una mafuta mengi tumboni au jinsi mtoto wako alivyolala.
Kwa maendeleo ya mtoto tumboni mimba ikiwa na miezi minne, mtoto anakuwa na urefu wa takribani inci 4 mpaka 5.
Pia sehemu za siri za mtoto zinakuwa tayari zimekuwa na kama utafanya kipimo cha ultrasound kwa mimba ya miezi minne unaweza kujua mtoto ni wa jinsia gani.
Jambo jingine kwa mtoto aliyeko tumboni kwa mimba ya miezi minne anakuwa na uwezo wa kusikia sauti,
unaweza kuongea na mwanao tumboni ili aanze kuizoea sauti yako na kuanzisha mausiano mazuri na mwanao akiwa bado yuko tumboni.
Unaweza pia kusoma: