Muonekano wa Giza:

Msaada

Pichani anaonekana mwanamke mjauzito akiwa amelala kwenye kochi huku akiwa ameshikilia tumbo lake.

Mimba ya miezi nane inakuaje?

Shauku ya wajawazito wengi ni kutaka kujua maendeleo ya mimba toka siku anajigundua kuwa ni mjamzito mpaka siku ya kujifungua.
Ili kufahamu hayo yote kuhusu maendeleo ya mimba kwanzia mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa tisa, fuatilia tovuti yetu kufahamu zaidi.
Katika makala hii tufahamu kuhusu mimba ya miezi nane inakuaje.
Kama una mimba ya miezi nane tarajia mambo haya yafuatayo:

Kuwa na mawazo mengi katika kipindi cha mimba ya miezi nane ni kawaida.
Wengi huwa na mawazo ya kupata mtoto siku za karibuni na kumaliza safari yake ya ujauzito.
Huanza kufikiria jinsi ya kuwa mlezi bora kwa mtoto wake.
Kukaa na kuzungumza na marafiki kunasaidia kupoteza mawazo hayo.

Kwa mimba ya miezi nane huhisi uchovu sana, tumia muda mwingi kupumzika.

Pia kwa mimba ya miezi nane mjamzito anaweza kupata shida ya kupumua, Hii ni kutokana na kutanuka kwa mfuko wa kizazi unaominya mapafu kwa mama mjamzito.

Kukojoa mara kwa mara, hii ni kwasababu ya mtoto kushuka chini na kuminya kibofu cha mkojo.

Kuhisi mgandamizo kwenye nyonga, ni kwasabu ya uzito wa mtoto kuongezeka na kushuka chini kwenye nyonga.

Michirizi kwenye tumbo, ni kwasababu tumbo linazidi kutanuka kama hupendi hali hiyo kuna baadhi ya lotion na cream zinaondoa michirizi hiyo.
Wakati mwingine wajawazito huisi mgandamizo wa misuli ya mfuko wa kizazi kama dalili ya uchungu lakini sio endelevu.
Hali hiyo ni ya kawaida kwa mimba ya miezi nane na huisha pale ambapo utabadilisha mkao wako.
Kuvumba kwa mishipa ya damu hasa ya miguuni, wakati mwingine inaweza kuwa inawsha na kukusababishia maumivu.

Bawasili, kwa baadhi ya wajawazito wanaweza kupata tatizo la bawasiri kutokana na mishipa ya damu kwenye njia ya haja kubwa kuvimba.
Kula mboga za majani na kunywa maji kwa wingi kunaweza kukusaidia kuepukana na tatizo hilo.

Pia kuhisi kizunguzungu:

Na kuhisi uchovu:

Dalili hizo ni za kawaida kwa wajawazito na huisha mara baada ya kujifungua na zingine huisha tu baada ya siku kadhaa ila kama zitakufanya kuwa na hali mbaya sana ni vizuri kumuona daktari kwa msaada zaidi.
Pia kuwahi au kuchelea kuziona dalili hizi kabla au baada ya miezi husika isikupe presha kwasababu mimba huja tofauti kwa kila mtu na dalili hizi haziwezi kuwa sawa kwa kila mtu au kwa kila ujauzito wako.

Kwa maendeleo ya mtoto tumboni kwa mwezi wa 8 wa ujauzito viungo vya mtoto hukua kwa kasi sana kukamilisha ukuaji wake kwaajili ya kukabiliana na mazingira ya nje ya tumbo.
Mpaka kumalizika kwa mwezi wa nane wa ujauzito mtoto anakuwa amekua mpaka kufikia urefu wa inchi 16 na nusu mpaka inchi 12.
Kwa mimba ya miezi nane unaweza kuanza kuhisi mtoto akicheza kwa kidogo sana, hiyo ni kwasababu mtoto amekuwa mkubwa kiasi cha kujibana kwenye mfuko a kizazi hivyo kushinda kujiachia vizuri kucheza.

0
0
1