Mimba ya miezi mitano inakuaje?
Shauku ya wajawazito wengi ni kutaka kujua maendeleo ya mimba toka siku anajigundua kuwa ni mjamzito mpaka siku ya kujifungua.
Ili kufahamu hayo yote kuhusu maendeleo ya mimba kwanzia mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa tisa, fuatilia tovuti yetu kufahamu zaidi.
Katika makala hii tufahamu kuhusu mimba ya miezi mitano inakuaje.
Kama una mimba ya miezi mitano tarajia mambo haya yafuatayo:
Kwa mimba ya miezi mitano tarajia kuona unaongezeaka uzito na hapa dalili nyingi za awali ambazo zinawakondesha wengi kama vile kutapika zinakuwa zimeisha.
Pia unaweza kuwa na kiungulia:
Maumivu miguuni:
Kwasababu ya kukakamaa kwa misuli au kuvumba kwa mishipa ya damu.
Kuvimba miguu:
Kupata choo kigumu:
Kuongezeka kwa hali ya kupata kizunguzungu:
Maumivu ya kichwa:
Maumivu ya mgongo:
Mabadiliko kwenye ngozi, hasa kuongezeka weusi kwenye chuchu.
Mafua mazito:
Dalili hizo ni za kawaida kwa wajawazito na huisha mara baada ya kujifungua na zingine huisha tu baada ya siku kadhaa ila kama zitakufanya kuwa na hali mbaya sana ni vizuri kumuona daktari kwa msaada zaidi.
Pia kuwahi au kuchelea kuziona dalili hizi kabla au baada ya miezi husika isikupe presha kwasababu mimba huja tofauti kwa kila mtu na dalili hizi haziwezi kuwa sawa kwa kila mtu au kwa kila ujauzito wako.
Kwa mtoto tumboni mimba ya miezi mitano anakuwa amekuwa mpaka kufikia uefu wa inchi 6 mpaka 7.
Kwa mwezi wa tano wa ujauzito ngozi ya mtoto inakuwa inazalisha uteute mzito ambao unaikinga ngozi ya mtoto
isiathiriwe na majimaji ya kwenye chupa ya kizazi.
Pia ngozi inakuwa na nywele nyingi hivyo vyote hupotea mara tu baada ya mtoto kuzaliwa.
Pia mtoto kwa wakati huo anakuwa anajifunza jinsi ya kunyonya kwa kunyonya vidole vyake mwenyewe.
Unaweza pia kusoma: