Mimba ya mwezi mmoja inakuaje?
Inawezekana kwa sasa unaona mabadiliko kadhaa kwenye mwili wako na unashindwa kuelewa ni nini.
Au labda umechelewa kuona siku zako na unajihisi kuwa ni mjamzito.
Na kama umepima ujauzito na umejigundua kama ni mjamzito hongera ila ungependa kujua hali ambaayo unaweza kupitia kwa mimba
yako changa.
Basi umechagua sehemu sahihi kuzijua dalili mbalimbali kwa mjamzito mwenye mimba ya mwezi mmoja.
Kwa mimba ya mwezi mmoja unaweza usihisi dalili yoyote, ila kwa baadhi wanaweza kupata dalili zifuatazo:
Kukosa hedhi:
Kama ulikuwa kwenye mzunguko wako wa hedhi kawaida na ukaona umechelewa kupata hedhi au kokosa kabisa hedhi kwa huo mwezi ni dalili mojawapo ya kuwa ni mjamzito.
Mabadiliko ya Tabia:
Unapokuwa mjamzito mwili unakuwa na mabadiliko ya homoni ndani ya mwili.
Ongezeko la homoni ndani ya mwili linaweza kusababisha mabadiliko ya kitabia kwa mjamzito.
Unaweza kujiona una wasiwasi sana au una hasira sana kuliko kawaida.
Tumbo kujaa gesi:
Kwa sababu ya ongezeko la homoni za ujauzito mwilini unaweza kuhisi tumbo kujaa gesi.
Hali hoyo wengi huichanganya na hali ya kawaida wakati wa hedhi.
Uchovu:
Kwa mimba ya mwezi mmoja mjamzito huanza kujisikia hali ya uchovu sana ni kwasababu nguvu kubwa ya mwili inatumika kuandaa mazingira ya ukuaji wa mtoto tumboni.
Maumivu ya matiti:
Pia kutokana na ongezeko la homoni ndani ya mwili kwa mjamzito husababisha maumivu ya matiti kwa mimba ya mwezi mmoja.
Maumivu ya tumbo:
Kutokana na mabadiliko mbalimbali yanayotokea kwenye mfuko wa kizazi kujiandaa kutunza mtoto,
mjamzito anaweza kuhisi maumivu chini ya kitovu hiyo ni moja ya dalili ya mimba ya mwezi mmoja.
Kukojoa mara kwa mara:
Kutokana na mabadiliko mbalimbali ya homoni na ukuaji wa mtoto kenye mfuko wa kizazi kwa mimba ya mwezi mmoja mjamzito anaweza
kujikuta anakojoa mara kwa mara kuliko kawaida, hiyo pia ni dalili ya mimba ya mwezi mmoja.
Vitone vya damu:
Pia kama ni mimba ya mwezi mmoja unaweza kuona kwenye nguo yako ya ndani kuna vitone vya damu, kama utaona hali hiyo usiogope ni moja ya dalili za mimba ya mwezi mmoja.
Unaweza pia kusoma: