Mimba ya miezi saba inakuaje?
Shauku ya wajawazito wengi ni kutaka kujua maendeleo ya mimba toka siku anajigundua kuwa ni mjamzito mpaka siku ya kujifungua.
Ili kufahamu hayo yote kuhusu maendeleo ya mimba kwanzia mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa tisa, fuatilia tovuti yetu kufahamu zaidi.
Katika makala hii tufahamu kuhusu mimba ya miezi saba inakuaje.
Kama una mimba ya miezi saba tarajia mambo haya yafuatayo:
Maumivu ya nyonga na maumivu chini ya mgongo:
Wakati mwingine maumivu hayo huanzia chini ya mgongo na kushuka chini ya miguu, kukanda kwa maji ya moto au maji baridi unaweza kusaidia kuondoa maumivu hayo.
Ikiwa kama utahisi miguu inakufa gazi ni vizuri kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.
Na hali hiyo hupotea mara baada ya kujifungua.
Kupata choo kigumu:
Kupunguza hali hii kunywa maji kwa wingi kutakusaidia.
Wakati mwingine wajawazito huisi mgandamizo wa misuli ya mfuko wa kizazi kama dalili ya uchungu lakini sio endelevu.
Hali hiyo ni ya kawaida kwa mimba ya miezi saba na huisha pale ambapo utabadilisha mkao wako.
Uchovu:
Pia kuna baadhi kwa ujauzito wa miezi 7 wanaweza kuona damu kidogo au vitone vya damu vikitoka ukeni,
japo ni hali ya kawaida tu kwa ujauzito wa miezi 7 ila unaweza kumuona daktari kwa ushari zaidi kwasababu kutoka damu ukeni ni moja ya dalili ya hatari kwa mjamzito.
Dalili hizo ni za kawaida kwa wajawazito na huisha mara baada ya kujifungua na zingine huisha tu baada ya siku kadhaa ila kama
zitakufanya kuwa na hali mbaya sana ni vizuri kumuona daktari kwa msaada zaidi.
Pia kuwahi au kuchelea kuziona dalili hizi kabla au baada ya miezi husika isikupe presha kwasababu mimba huja tofauti kwa kila
mtu na dalili hizi haziwezi kuwa sawa kwa kila mtu au kwa kila ujauzito wako.
Kwa mwezi wa saba wa ujauzito mtoto tumboni mifumo yake ya mwili inakamilisha ukuaji ili kuweza kukabiliana na mazingira nje ya tumbo la mama.
Pia mtoto akiwa tumboni anaweza kuhisi mwanga au giza, wakati mwingine unaweza kuhisi mtoto anacheza unapotoka kwenye giza kuingia kwenye mwanga.
Na kwa mimba ya miezi saba mtoto anakuwa amekuwa mpaka kufikia urefu wa inchi 14.
Unaweza pia kusoma: