Ukuaji wa mtoto tumboni kwa mama mjamzito mwenye mimba ya miezi minne.
Mimba ni mchakato wa asili wa muda mrefu kwa binadamu, inachukua takribani siku 280 au wiki 40 ambayo pia inakadiriwa miezi 9 mpaka mtoto kuzaliwa na kuwa na uwezo wa kuyaishi mazingira ya nje ya tumbo la mama.
Mchakato huu kwa mtoto huanzia kwenye seli moja tu ambayo ni mchanganyiko wa yai la mama na mbegu ya baba.
Seli hiyo hugawanyika mpaka kupata mamilioni mengine ya seli ambazo huunda viungo mbalimbali ndani na nje ya mwili wa mtoto.
Kuna hatua mbalimbali ambazo mtoto tumboni anazipitia kutoka yai la mama kurutubishwa mpaka wakati wa kujifungua.
Tufahamu nini kinachoendelea tumboni kwa mama mjamzito katika miezi yake yote 9 mpaka kujifungua.
Kwa miezi minne ya ujauzito, mwili wa mtoto unaanza kukua kwa uwiano sawa na kichwa, kwasababu mwanzoni kichwa
huwa kikubwa sana kuliko mwili wa mtoto.
Katika miezi iliyopita ngozi ya mtoto inakuwa nyembamba sana na inayoangaza kiasi cha kuweza kuona viungo vyake vya ndani.
Katika kipindi hiki ngozi huongezeka unene na kupoteza uangavu wake.
Pia nywele kidogo zinaanza kuota.
Katika kipindi hiki mtoto anaanza kujifunza baadhi ya matendo kama vile kupeleka vidole yake mdomoni na kuzungusha kichwa chake.
Kwa miezi minne ya ujauzito jinsia ya mtoto inaweza kujulikana kwasababu viungo vyake vya uzazi nje ya mwili tayari vimekua kuweza kuonekana kwa ultrasound.
Masikio ya mtoto yanakuwa yamekua vya kutosha kiasi kwamba anaweza kusikia sauti ya mama yake akiwa anaongea.
Na macho yake japokuwa yanakuwa yamefunikwa na kope lakini ikitokea mwanga umemulikwa tumboni anaweza kujigeuza kuukwepa mwanga.
Mpaka kukailika mwezi huu wa nne, mtoto anakuwa amekuwa mpaka kufikia takribani inchi 4.5 urefu wake kutoka kichwani mpaka kwenye makalio.
Moja kati ya kipindi cha furaha kwa wajawazito wengi ni kipindi hiki cha miezi minne ya ujauzito.
Baadhi ya dalili zilizokuwa zinasumbua miezi mitatu iliyopita zinaweza kuwa zimepotea.
Hali ya kichefuchefu kwa mjamzito inaweza kuwa imepungua katika kipindi hiki.
Hali nyingine kama vile kiungulia na kupata choo kigumu zinaweza kuendelea au kuongezeka katika kipindi hiki.
Pia matiti yanaendelea kuongezeka pamoja na kupata maumivu ya matiti.
Ongezeko la damu mwilini kwa mama mjamzito ili kukidhi mahitaji ya mtoto tumboni inaweza kusababisha baadhi ya madhara kwa
mama mjamzito.
Baadhi ya madhara hayo ni kama vile, kutokwa na damu puani au kutokwa na damu kwenye fizi.
Pia wakati mwingine inaweza kusababisha mama mjamzito kupata hali ya kizunguzungu.
Unaweza pia kusoma: