Kutokwa na damu ukeni kwa mjamzito kabla ya miezi minne (Inamaanisha nini? Ni dalili ya nini?)
Kutokwa na damu ukeni wakati wa ujauzito inaweza kuwa ni hali ya kawaida kwa mjamzito ila haipaswi kuchukulia poa hali hiyo kwasababu kutokwa na damu ukeni ni moja ya dalili za hatari kwa mjamzito.
Kama ni mjamzito na unaona damu zinatoka ukeni katika hali yoyote ile ni muhimu kufika hospitali haraka kwa uchunguzi zaidi.
Katika makala hii tuzifahamu sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha kutokwa na damu ukeni kwa mjamzito hasa kwa mimba changa chini ya miezi 4.
Kijusi kujishikiza kwenye kuta za mfuko wa kizazi:
Moja ya sababu za mjamzito kutokwa na damu ukeni wakati wa mimba changa ni kijusi kujishikiza kwenye kuta za kizazi.
Baada ya mbegu za kiume na yai la mwanamke kukutana kijusi kinachopatikana huchimba na kujishikiza kwenye kuta za kizazi ili kuendelea kukua.
Hali hiyo inaweza kusababisha damu kidogo au vitone vya damu kutoka ukeni wakati wa mimba changa.
Mabadiliko kwenye shingo ya kizazi.
Mimba inaweza kusababisha mabadiliko kadhaa kwenye shingo ya kizazi.
Mabadiliko hayo yanaweza kusababisha kutokwa na damu ukeni wakati wa ujauzito, mfanno damu inaweza kutoka baada ya tendo la ndoa.
Dalili za mimba kutoka au kutunga nje ya kizazi.
Moja ya dalili ya mimba kutaka au kutishia kutoka ni kutokwa na damu ukeni kwa mjamzito mimba ikiwa bado changa.
Pia ni dalili ya mimba iliyotunga nje ya mfuko wa kizazi.
Hivyo zingatia kuwa kutokwa na damu ukeni wakati wa ujauzito ni moja ya dalili hatari kwa mjamzito ni muhimu kuwahi kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi.
Unaweza pia kusoma: