Mjamzito usifanye mapenzi au tendo la ndoa kama ukiona mambo haya
Kufanya mapenzi wakati wa ujauzito ni salama kwa mjamzito kwasababu hakuna tafiti yoyote ya kisayansi iliyothibitisha madhara kwa wajawazito.
Sio wakati wote mjamzito anapaswa kufanya mapenzi ila kuna baadhi ya sababu zinazomzuia mjamzito kushiriki tendo la ndoa kabisa kwa usalama wa mimba.
Pia kuna faida ambazo mjamzito anaweza kuzipata akishiriki tendo la ndoa.
Faida za kufanya mapenzi au kufanya tendo la ndoa ukiwa mjamzito
Katika makala hii tuzifahamu sababu ambazo mjamzito akiziona au zikigundulika kwa mjamzito hashauriwi kabisa kushiriki tendo la ndoa.
Sababu hizi mjamzito anaweza kuziona mwenyewe au baada ya vipimo vya hospitali.
Sababu hizo ni kama ifuatavyo:
- Kutokwa na damu ukeni bila sababu yoyote kipindi cha ujauzito.
- Kupasuka kwa chupa ya uzazi au kutokwa na maji ukeni wakati wa ujauzito.
- Kuanza kutanuka kwa shingo ya kizazi mapema kabla ya muda wa uchungu kuanza.
- Kondo likijishikiza kwenye tundu la shingo ya kizazi kwa sehemu ndogo au likiziba kabisa tundu la shingo ya kizazi.
- Kama una historia ya nyuma ya kupata uchungu mapema kabla ya muda au kujifungua mapema kabla ya muda.
- Na Kama una mimba ya mapacha.
Unaweza pia kusoma: