Muonekano wa Giza:

Msaada

Picha inayoonesha mwanamke amelala kitandani akiwa kwenye dimbwi la mawazo baada ya ujauzito wake kutoka.

Nini cha kufanya baada ya kutoa au mimba kuharibika

Mimba itahesabika kama mimba iliyoharibika au iliyotoka kama itatoka au kuharibika kabla ya wiki ya 28 ya ujauzito.
Mimba inaweza kuharibika bila kukusudia kwasababu kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha mimba kuharibika.
Pia kuna wengine hutoa mimba kwa makusudi kwa kutumia njia mbalimbali kama vile kutumia vifaa kuchokonolea au kwa kutumia madawa.
Katika makala hii tufahamu mambo kadhaa muhimu ya kuyazingatia mwanamke kama mimba imeharibika au kutoka.

Kupata Mapumziko:
Kama mimba imetoka mwanamke anaweza kuwa amepoteza damu nyingi, kutokana na kupungukiwa damu mwilini mwili unakosa nguvu.
Mwili unahitaji kupumzika vya kutosha ili kupata nafasi ya kujirejesha katika hali yake ya kawaida.

Usafi ukeni:
Ni kawaida kwa mwanamke kutokwa na damu ukeni kwa wiki kadhaa baada ya mimba kutoka.
Hakikisha unabadilisha pedi kila baada ya masaa 4 au 6.
Pia ni muhimu kusafisha vizuri ukeni mara kwa mara.
Na usifanye tendo la ndoa au kuingiza kitu chochote ukeni wakati damu bado inaendelea kutoka subiri ikate.

Uzazi wa mpango:
Ili kizazi kikae sawa kubeba mimba nyingine inashauriwa wanamke kukaa angalau miezi sita baada ya mimba kutoka.
Ili kuweza kujilinda kwa kipindi chote hicho kushika ujauzito ni muhimu kutumia njia za uzazi wa mpango.
Nenda kituo cha afya kupata ushauri ni njia ipi bora ya uzazi wa mpango inakufaa kutumia kwa kipindi hicho cha miezi sita.

Pia mwanamke anapoona dalili zifuatazo ni muhimu kuwahi hospitali haraka iwe usiku au mchana kwa msaada zaidi.
- Damu kuongezeka kutoka kwa siku mbili mfululizo.
- Homa kali.
- Kuhisi kizunguzungu au kuzimia.
- Maumivu makali ya tumbo.
- Maumivu ya mgongo.
- Kichefuchefu na kutapika.
- Kutokwa na uchafu ukeni unaotoa harufu baya.

0
0
1