Muonekano wa Giza:

Msaada

Picha inamuonesha mtoto ambaye yupo tumboni kwa mama yake ajazaliwa bado.

Ukuaji wa mtoto tumboni kwa mama mjamzito mwenye mimba ya miezi nane.

Mimba ni mchakato wa asili wa muda mrefu kwa binadamu, inachukua takribani siku 280 au wiki 40 ambayo pia inakadiriwa miezi 9 mpaka mtoto kuzaliwa na kuwa na uwezo wa kuyaishi mazingira ya nje ya tumbo la mama.

Mchakato huu kwa mtoto huanzia kwenye seli moja tu ambayo ni mchanganyiko wa yai la mama na mbegu ya baba.
Seli hiyo hugawanyika mpaka kupata mamilioni mengine ya seli ambazo huunda viungo mbalimbali ndani na nje ya mwili wa mtoto.

Kuna hatua mbalimbali ambazo mtoto tumboni anazipitia kutoka yai la mama kurutubishwa mpaka wakati wa kujifungua.
Tufahamu nini kinachoendelea tumboni kwa mama mjamzito katika miezi yake yote 9 mpaka kujifungua.

Kwa miezi nane ya ujauzito mtoto tumboni anaendelea kukua na mwili wake unaendelea kuzalisha mafuta kwa wingi.
Mafuta ambayo yanamsaidia mtoto kuwa na uwezo wa kuthibiti joto la mwili wake.

Ubongo wa mtoto unaendelea kukua na kukomaa kwa kasi katika kipindi hiki na uwezo wa mtoto kuona na kusikia nao unakuwa umeongezeka.

Katika kipindi hiki mama anaweza kujua muda wa mtoto tumboni kulala au kuamka kwasababu ana uwezo wa kuzihisi purukushani za mtoto wake vizuri.

Ngonzi ya mtoto inakuwa si ang'avu tena katika kipindi hiki.
Na viungo vyake mwilini kasoro mapafu na ubongo vinakuwa vimekamilisha ukuaji wake kuwa tayari kuzaliwa.

Viungo vyote ndani ya mwili wa mtoto kasoro Ubongo na mapafu vinakuwa vimekomaa na kuwa na uwezo wa kufanya kazi nje ya tumbo la mama.

Mpaka mwishoni mwa mwezi wa nane urefu wa mtoto ni wastani wa inchi 17 mpaka 18 na uzito wa wastani mpaka kilo 2.

Kwa mama mjamzito mwenye mimba ya miezi nane huhisi uchovu sana, tumia muda mwingi kupumzika.

Pia kwa mimba ya miezi nane mjamzito anaweza kupata shida ya kupumua, Hii ni kutokana na kutanuka kwa mfuko wa kizazi unaominya mapafu kwa mama mjamzito.

Kukojoa mara kwa mara, hii ni kwasababu ya mtoto kushuka chini na kuminya kibofu cha mkojo.

Kuhisi mgandamizo kwenye nyonga, ni kwasabu ya uzito wa mtoto kuongezeka na kushuka chini kwenye nyonga.

Kwa baadhi ya wajawazito wanaweza kupata tatizo la bawasiri kutokana na mishipa ya damu kwenye njia ya haja kubwa kuvimba.
Kula mboga za majani na kunywa maji kwa wingi kunaweza kukusaidia kuepukana na tatizo hilo.

0
0
1