Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Chai ya kijani tiba asili ya uvimbe kwenye kizazi

Chai ya kijani ni aina ya chai ambayo huandaliwa kwa kutumia majani ya chai ambayo huchumwa moja kwa moja kutoka kwenye mti wa chai kabla ya kuchakatwa kiwandani.

Asili ya chai ya kijani ni china licha ya kutumiwa kama kinywaji pia chai ya kijani imeonekana kuwa na virutubisho vingi muhimu kwa afya kuliko chai ya kawaida nyeusi.

Chai ya kijani imetanjwa na wataalamu mbalimbali kuwa ni moja kati ya vinywaji vyenye faida nyingi za kiafya.

Moja kati ya kirutubisho muhimu kwenye chai ya kijani ni EGCG yani Epigallocatechin Gallate.
Kirutubisho hiki tafiti zimeonesha kuwa ni muhimu kwasababu ya uwezo wake wa kuondoa sumu mwilini na kuzuia uharibifu wa seli ndani ya mwili.

Pia tafiti zimeonesha kirutubisho cha EGCG kinasaidia kuondoa uvimbe sehemu mbalimbali za mwili pia kinasaidia kuukinga mwili na magonjwa ya muda mrefu kama vile magonjwa ya moyo, kisukari na baadhi ya saratani mwilini.
Kirutubisho hichohicho pia kimeonekana kuwa na msaada kwa wanawake wenye tatizo la uvimbe kwenye kizazi.

Inakadiriwa kati ya asilimia 20 mpaka 80 ya wanawake wanaweza kuwa wamepata uvimbe kwenye kizazi mpaka kufikia miaka 50.
Asilimia 99 ya uvimbe kwenye kizazi haisababishi madhara makubwa ya kiafya.

Kuna baadhi ya vimbe kwenye kizazi zinaweza zisionekane na baadae hupotea zenyewe bila matibabu yoyote pia kuna baadhi ni kubwa kiasi cha kuweza kuguusa kwa kupapasa tumbo.

Uvimbe unaweza kuwa mmoja au vimbe zaidi ya moja sehemu tofauti tofauti kwenye kizazi.
Dalili za uvimmbe kwenye kizazi hutofautiana kulingana na ukubwa wa uvimbe, mahali ulipo na idadi ya vimbe kwenye kizazi.

Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa chai ya kijani inaweza kusaidia kupunguza ukubwa wa uvimbe na dalili za uvimbe kwenye kizazi.

Majani baada ya kuchumwa mtini hukaushwa kidogo juani ili kupunguza maji maji kwenye majani kabla ya kuyatumia kuandalia chai.
Hakikisha kwa siku unakunywa vikombe visivyozidi 8 kwa afya.

Kwasababu ya uwepo wa caffeine kwenye chai ya kijani inaweza kuleta maudhi mbalimbali mwilini kama vile kichwa kuuma.

Chai ya kijani haushauriwi kunywa kabla ya kula kitu chochote kwa mujibu wa tafiti mbalimbali inaweza kusababisha matatizo ya ini.
Kama ni mjamzito au kama unanyonyesha haishauriwi kutumia chai ya kijani kwasababu ya uwepo wa caffeine kwenye chai ya kijani.

0
0