Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Kabla ya kunywa Asali zingatia mambo haya

Asali hiki ni kimiminika cha asili kinacho tengenezwa na nyuki kwa mkusanyiko wa nectar kutoka kwenye mimea tofauti tofauti inayotoa maua.

Licha ya kuwa na sukari nyingi ina uchache wa mafuta, protini na nyuzi lishe, asali pia ina wingi wa virutubisho vingine muhimu kwa afya kutoka kwenye mimea tofautitofauti.

Asali imekuwa ikitajwa sana kuwa ni moja kati ya vinywaji vya asili vyenye faida nyingi za kiafya kwa binadamu na kutumiwa kama tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya.

Na tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa asali inasaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo, ni tiba ya kifua, tiba ya matatizo ya tumbo kama tumbo kuuma au kuharisha, pia asali inasaidia kuponesha vidonda hasa vya kuungua na moto.

Chenye faida hakikosi kuwa na hasara zake.

Kuna baadhi ya mambo ni muhimu kuyazingatia kabla ya kutumia asali kama tiba au kwa matumizi yako mengine.

Tafiti mbalimbali za kisanyansi zimeonesha kuwa asali ni salama kutumiwa na watu wazima na watoto wenye umri wa zaidi ya mwaka mmoja.

Kamwe usijaribu kumpa au kumlambisha hata kiasi kidogo tu cha asali mtoto aliye chini ya mwaka mmoja.
Watoto chini ya mwaka mmoja utumbo wao hauna kinga ya kudhibiti bakteria ambao wanaweza kupatikana kwenye asali.
Hata kiasi kidogo tu cha asali kwa mtoto chini ya mwaka mmoja kinaweza kumsababishia matizo makubwa ya tumbo.

Kuna baadhi ya watu wana allergy na mbelewere, na nyuki ni moja kati ya wadudu wanaotembelea maua na kukusanya mbelewere tofautitofauti.
Japo kwa uchache ila mbelewere kwenye asali zinaweza kusababisha matatizo makubwa kwa mtu mwenye allergy.

Ikiwa utatumia asali na kupata dalili kama vile:

Ni muhimu kuacha matumizi ya asali na muone daktari kwa msaada zaidi.

0
0