
Changanya Tangawizi, Karafuu, Limao na Asali upate faida hizi kwa afya
Tengeneza chai iliyo changanywa karafuu na Tangawizi ichemke angalau kwa dakika 5 mpaka 10,
Kamulia kipande cha Limao kwenye kikombe kimoja cha chai na kisha utumie asali kama sukari yako kwenye chai hiyo.
Kutumia chai hiyo mara kwa mara inaweza kukupa faida hizi zifuatazo kwa afya yako.
Inasaidia kusafisha mwili.
Kunywa chai hii mara kwa mara inasaidia kuondoa kemikali hatari mwilini na kuzilinda seli za mwili zisiharibiwe na kemikali hizo.
Kusafisha mwili itakusaidia kukukinga na magonjwa ya muda mrefu na yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari na magonjwa ya moyo.
Pia itakusaidia kuimarisha afya ya ngozi yako na kuzuia dalili za uzee kuonekana mapema kama vile makunyanzi.
Ni kinga dhidi ya saratani.
Baadhi ya virutubisho kwenye chai hii vimeonekana kuwa na uwezo wa kudhibiti ukuaji wa seli za saratani mwilini.
Unywaji wa chai hii mara kwa mara unakuongezea kinga dhidi ya saratani mwilini.
Ni kinga ya mawe kwenye figo.
Kwa msaada wa citric acid inayopatikana kwa wingi kwenye limao itakusaidia kukukinga na tatizo la mawe kwenye figo.
Inasaidia kuimarisha afya ya ubongo.
Wingi wa madini ya manganese kwenye karafuu unasaidia kuimarisha afya ya ubongo pamoja na virutubisho vingine kwenye Tangawizi
vimeonekana kusaidia kuimarisha utendaji kazi wa ubongo.
Vinasaidia kuimarisha uwezo wako kufikiri na kutunza kumbukubu.
Pia ni kinga ya tatizo la kupoteza kumbukumbu linalosababishwa na kufa kwa seli za ubongo hasa kwa wazee.
Inasaidia kuimarisha afya ya moyo.
Chai hii itaupa mwili wako vitamin C kwa wingi vitamin ambayo imeonekana kusaidia kuimarisha afya ya moyo.
Pia virutubisho vingine kwenye chai hii vimeonekana kusaidia kupunguza mafuta mabaya ya cholesterol mwilini ambayo
ni hatari kwa afya ya moyo.
Inasaidia kuimarisha mifupa na kuondoa maumivu ya joints.
Karafuu ina wingi wa madini ya manganese ambayo yanasaidia kuongeza ujazo kwenye mifupa na kuifanya iwe imara.
Na kama unasumbuliwa na maumivu kwenye viungo vya mwili Virutubisho kwenye chai hii pia vinasaidia kupunguza maumivu hayo.
Tiba ya kuvimbiwa.
Karafuu na tangawizi zinasaidia kuchochea umeng’enywaji wa chakula kwenye mfumo wa chakula.
Kasi ya chakula kupita kwenye utumbo itaongezeka na kukuondolea dalili za kuvimbiwa kwa haraka.
Inasaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu.
Chai hii ni muhimu kwa wenye kisukari kwasababu inasaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu hasa inapotumiwa baada ya kula.
Inasaidia kuchochea uzalishaji wa homoni ya insulin mwilini na kuchochea ufyonzaji wa sukari kutoka kwenye damu kwenda kwenye
seli za mwili kwa matumizi yake ya kawaida.
Inasaidia kuua baadhi ya bakteria hatari mwilini.
Karafuu, Tangawizi na Asali virutubisho vyake vimeonekana kuwa na uwezo wa kuua baadhi ya bakteria hatari mwilini hasa bakteria
wanaosababisha matatizo ya meno na kinywa, wanaosababisha magonjwa ya tumbo na magonjwa ya ngozi.
Pia virutubisho kwenye Karafuu na Tanagawizi vimeonekana kuwa na uwezo wa kutibu fangasi hasa aina ya candida wanaosababisha fangasi mdomoni na ukeni.
Kinga na tiba ya upungufu wa Damu.
Citric acid na vitamin C kwenye chai hii vinasaidia kuchochea ufyonzaji wa madini chuma kutoka kwenye chakula kwenda kwenye damu
kwaajili ya uzalishaji wa seli nyekundu za damu kwa wingi.
Kama una upungufu wa damu unaosababishwa na upungu wa madini chuma chai hii ni msaada kwako.
Unaweza pia kusoma: