Muonekano wa Giza:

Msaada

Picha inamuonesha kijiko cha mbao chenye mchanganyiko wa kitunguu saumu na tangawizi zilizosagwa na pembeni yake kuna kipande cha tangawizi na kitunguu saumu kimoja.

Changanya kitunguu saumu na tangawizi upate faida hizi kwa afya yako.

Kitunguu saumu na Tangawizi ni viungo vya chakula maarufu sana duniani kutokana na wingi wa virutubisho vyake muhimu kwa afya ya binadamu.
Kitunguu saumu na Tangawizi hutumika sana kwa kuongeza ladha nzuri na harufu nzuri ya chakula.

Pia tafiti mbalimbali za kisayansi zilifanywa kwenye viungo hivyo nakugundulika kuwa na virutubisho mbalimbali muhimu kwa afya.
Virutubisho vyake vilionekana kusaidia kuthibiti vichocheo vya magongwa, kusafisha sumu mwilini na kuongeza kinga ya mwili kupambana na magonjwa mbalimbali.

Mchanganyiko wa Kitunguu saumu na Tangawizi umeonekana pia kuwa na wingi wa faida kwa afya yako.

Unaweza kuutumia mchanganyiko huo kwa namna mbalimbali, unaweza kutumia kwa kuvichanganya viungo hivyo kwenye chakula au supu.
Pia unaweza kuvitumia viungo hivyo pamoja kwenye chai asubuhi.

Ili kuvipata virutubisho vyake vyote ni vizuri kuvitumia vibichi au kuvipika kwenye mto kidogo.
Kukaa kwenye moto kwa muda mrefu inaweza kusababisha kuharibu baadhi ya virutubisho.

Ni kiasi gani cha kutumia mchanganyiko huu?

Kwa kitunguu saumu na tangawizi vilivosagwa chota vijiko viwili vya chai vya kitunguu saumu na vijiko viwili vya chai vya tangawizi.
Unaweza kuchanganya kwenye chai, juisi ya matunda au supu.
Mchanganyiko huu unautumia kwa siku mara mmoja.
Ili kupata matokeo mazuri unaweza kutumia mfululizo kwa wiki 12 (Miezi 3).

Zifuatazo ni faida za kutumia mchanganyiko wa Kitunguu saumu na Tangawizi kwa afya.

Unasaidia kupunguza vichocheo vya magongwa.

Moja kati ya faida ya virutubisho vya kitunguu saumu na tangawizi ni uwezo wake wa kupunguza vichocheo vya magonjwa mwili.
Inasaidia kupunguza homa za mara kwa mara na maumivu ya viungo sehemu mbalimbali za mwili.

Unasaidia kuzuia uharibifu wa seli mwilini.

Faida nyingine ya mchanganyiko wa kitunguu saumu na tangawizi ni kusaidia kuondoa sumu mwilini.
Kuondoa sumu mwilini kunaziweka seli za mwili katika usalama kuzikinga zisiharibiwe na sumu hizo.
Pia hali hiyo inasaidia kuukinga mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari na magonjwa ya moyo.

Unasaidia kuimarisha afya ya ubongo.

Tafiti zimeonesha kuwa matumizi ya mara kwa mara ya Tangawizi na Kitunguu saumu husaidia kuimarisha afya ya ubongo na kuongeza uwezo wa mtu kufikiri na kufanya maamuzi kwa wepesi.
Pia tafiti zimaonesha matumizi ya mchanganyiko huu inasaidia kuimarisha uwezo wa mtu kutunza kumbukumbu.

Unasaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo.

Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa matumizi ya mara kwa mara ya mchanganyiko wa kitunguu saumu na tangawizi inasaidia kupunguza hatari ya mtu kupata magonjwa ya moyo kwasababu inasaidia:

Ni msaada kwa watu wenye tatizo la kisukari.

Kitunguu saumu na Tangawizi zimeonekana kuwa na msaada kwa watu wenye tatizo la kisukari kwa kusaidia kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu.
Katika utafiti uliofanywa mwaka 2020 watu wenye tatizo la kisukari walipewa virutubisho vya tangawizi kwa siku 90 mfululizo walionekana kupunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha sukari kwenye damu.

Ni kinga dhidi ya saratani.

Baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa Tangawizi na Kitunguu saumu zina baadhi ya virutubisho ambavyo vinaweza kuukinga mwili dhidi ya baadhi ya saratani.
Kitunguu saumu kimeonekana kupungunza hatari ya kupata saratani ya matiti na Tangawizi imeonekana kupunguza hatari ya kupata saratani ya mapafu na saratani ya tumbo.

Unasaidia kuongeza kinga ya mwili.

Mchanganyiko wa Kitunguu saumu na Tangawizi una wingi wa virutubisho vinavyosaidia kuondoa vichocheo vya magonjwa, kuondoa sumu mwilini na kupambana na vimelea mbalimbali vya magonjwa.
Kwasababu hiyo unasaidia kuweka mwili salama na kuongeza kinga ya mwili.

Mwisho:

Faida hizi ni kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisayansi, Tangawizi na Kitunguu saumu kila kimoja kina faida zake kwa afya.
Kuchanganya vyote kwa pamoja kunaongeza wingi wa virutubisho vyake mwilini na kuupa mwili faida zaidi za kiafya.

Matumizi ya kitunguu saumu au Tangawizi yanaweza kuingilia matibabu ya hospital, hivyo kama unatumia dawa za hospitali na unataka kutimia mchanganyiko huu kwa tiba ni vizuri kumueleza daktari wako kwanza kabla ya kutumia.

0
0
1