
Mchanganyiko wa kitunguu saumu na asali uliovundikwa una faida gani kwa afya?
Kitunguu saumu ni moja kati ya viungo maarufu duniani kutokana na ukali wa harufu yake unaotumika kwenye mapishi pia kutokana na wingi wa virutubisho vyake muhimu kwa afya ya binadamu.
Kitunguu saumu peke yake kimeonekana kusaidia kama kinga ya magonjwa ya moyo, kinga dhidi ya saratani, na kinga ya magonjwa ya uzeeni.
Asali hiki ni kimiminika cha asili kinacho tengenezwa na nyuki kwa mkusanyiko wa nectar kutoka kwenye mimea tofauti tofauti inayotoa maua.
Asali imekuwa ikitajwa sana kuwa ni moja kati ya vinywaji vya asili vyenye faida nyingi za kiafya kwa binadamu na kutumiwa kama tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya.
Kitunguu saumu na asali tafiti mbalimbali zimethibitisha kuwa vina faida nyingi za kiafya kwa binadamu.
Unaweza kufaidika kwa kutumia kimoja kimoja au vyote kwa pamoja.
Na hizi ni baadhi ya faida ambazo mtu anaweza kuzipata kwa kutumia kitunguu saumu na asali kwa pamoja.
Baada ya tafiti mbalimbali kufanywa kwa mchanganyiko wa kitunguu saumu na asali imegundulika kuwa.
1. Kitunguu saumu na asali vinaweza kuzuia ukuaji wa baadhi ya bakteria hatari mwilini.
Mchanganyiko huo una uwezo wa kuzuia ukuaji wa bakteria hasa wanaoweza kusababisha homa ya mapafu na bakteria wanaosababisha sumu kwenye chakula.
Pia mchanganyiko huo tafiti zimeonesha una uwezo wa kuzuia hata bakteria wengine ambao dawa za kawaida za hospital haziwezi kuzuia.
Na si tu kuwa na uwezo wa kuzui bakteria pia tafiti zinaonesha kuwa mchanganyiko wa asali na kitunguu saumu una uwezo wa kudhibiti baadhi ya virusi mwilini.
2. Mchanganyiko huu unaweza kusaidia kutibu mafua na magonjwa mengine yanayosababisha na virusi.
3. Kitunguu saumu na Asali ni kinga dhidi ya magonjwa ya moyo.
Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa mchanganyiko wa asali na kitunguu saumu ni kinga ya magonjwa ya moyo na kiharusi kwasababu zifuatazo:
- Unasaidia kusafisha mwili.
- Unasaidia kushusha shinikizo la damu au presha.
- Unasaidia kupunguza mafuta mabaya ya cholesterol mwilini.
- Unazuia damu kuganda hovyo hovyo kwenye mishipa ya damu.
- Unazuia kukakamaa kwa mishipa ya damu ili kurushusu damu kupita kirahisi.
4. Mchanganyiko wa asali na kitunguu saumu unasaidia kuimarisha afya ya ubongo na kutunza kumbukumbu.
Machanganyiko wa asali na kitunguu saumu ni muhimu sana hasa kwa wazee kwasababu unasaidia kuongeza kinga mwili na kuzuia magonjwa.
Pia unasaidia kuimarisha afya ya ubongo na ni kinga ya matatizo ya kupoteza kumbukumbu.
Jinsi ya kuandaa mchanganyiko huu tafuta kopo au chupa ambayo ina mfuniko imara ambao hauwezi kuruhusu hata hewa kuingia ndani.
Hakikisha ni safi au ichemshe kwenye maji ya moto kuua vijidudu kwenye chupa.
Menya kitunguu saumu na uvikate vipande vyake nusu nusu kisha viweke kwenye chupa.
Tumia asali mbichi peke yake mimina kwenye chupa uchange na vitunguu saumu.
Funika chupa vizuri hakikisha hakuna kinachotoka wala kuingia kwenye chupa hiyo.
Huifadhi mchangayiko huo kwa kuigeuza chupa ili sehemu ya mfuniko ikae chini.
Huifadhi kwa wiki mbili ila kila siku hakikisha unafungua kidogo chupa ili kutoa gesi zitakazokuwa zimejikusanya kwenye chupa.
Unapoifungua hakikisha haikai muda mrefu wazi, fungua kidogo kuruhusu tu gesi kutoka na ufunike tena, igeuze chupa na endelee kuifadhi.
Baada ya wiki 2 inafaa kwa matumizi ila ili iwe bora zaidi inashauriwa kuifadhi kwa mwezi mzima.
Kutoka kwenye mchanganyiko huo unaweza kutumia punje moja moja ya kitunguu saumu kila siku au kijiko cha chai kimoja cha asali kila siku.
Tafuna punje 2 za Kitunguu saumu na punje 4 za Karafuu Upate faida hizi kwa afya yako
Kabla ya kunywa Asali zingatia mambo haya
Unaweza pia kusoma: