Tafuna Punje mbili za kitunguu saumu asubuhi kabla ya kula kitu upate faida hizi kwa afya yako
Inashauriwa kuwa kutumia kitunguu saumu kibichi ni bora zaidi kuliko kilichopikwa kwasababu baadhi ya virutubisho kwenye kitunguu saumu vina-haribiwa na joto kali.
Punje 1 au 2 za kitunguu saumu zinatosha kuupatia mwili wako virutubisho vyake muhimu kwa afya yako.
Ili kuvipata virutubisho vyake vizuri pia inashauriwa kutafuna angalau punje 2 za kitunguu saumu mapema asubuhi kabla hujala kitu chochote.
Ufyonzaji wa virutubisho mwilini umeonekana kuwa bora zaidi ukikitafunaa kulilo ukimeza bila kutafuna.
Kama utashindwa kuvumilia harufu yake mdomoni unaweza kukata punje ya kitunguu saumu vipande vidogo viache mezani kwa dakika 10 kabla ya kuvimeza na kushushia na glasi ya maji.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisayansi hizi ni baadhi ya faida za kiafya unazoweza kuzipata kutoka kwenye punje hizo 2 za kitunguu saumu.
Ni chanzo kizuri cha vitamin na madini muhimu mwilini.
Vitamin B6 na Vitamin C, Madini ya Manganese na Selenium hupatikana kwa wingi kwenye kitunguu saumu.
Pia ni chanzo kizuri cha nyuzi lishe.
Inasaidia kuongeza kinga ya mwili.
Baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa kitunguu saumu kinasaidia kuongeza kinga ya mwili na kuongeza uwezo wa
mwili kupambana na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza.
Pia kimeonekana kuwa na msaada zaidi kama kinga ya mafua kinapotumiwa msimu wa homa za mafua.
Inasaidia kudhibiti shinikizo la damu.
Tafiti zimeonesha kuwa virutubisho kwenye kitunguu saumu vinasaidia kushusha shinikizo la damu kwa
watu wenye shinikizo la juu la damu.
Virutubisho hivyo vinasaidia kudhibiti uzalishaji wa homoni ya angiontensin II ambayo inachangangia
kuongeza shinikizo la damu na vinasaidia kutanua mishipa ya damu kuruhusu damu kupita kirahisi.
Inasaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo.
Moja kati ya msaada wa kitunguu saumu ni kusaidia kupunguza mafuta mabaya ya cholesterol mwilini, mafuta ambayo yanaweza kuganda kwenye mishipa ya damu na kusababisha shida ya moyo kusukuma damu.
Inasaidia kusafisha mwili.
Virutubisho kwenye kitunguu saumu vinasaidia kusafisha mwili kwa kuondoa kemikali hatari mwilini na
kuzilinda seli za mwili zisiharibiwe na kemikali hizo.
Pia virutubisho hivyo vimeonekana kuwa na msaada wa kuzilinda seli za ubongo na kupunguza hatari ya kupata
tatizo la kupoteza kumbukumbu hasa kwa wazee.
Inasaidia kupunguza uchovu na maumivu ya misuli kwa wafanya mazoezi.
Inasaidia kuimarisha mifupa.
Tafiti zimeonesha kuwa kitunguu saumu ni msaada hasa kwa wanawake ambao wamefikia ukomo wa hedhi kwasababu
kinasaidia kuimarisha afya yao ya mifupa.
Pia kitunguu saumu kimeonekana kusaidia kupunguza maumivu kwa wanawake wenye maumivu ya joints na wenye uzito mkubwa.
Unaweza pia kusoma: