Muonekano wa Giza:

Msaada

Picha inamuonesha mwanamke akiwa ameachama mdomo wake na akiwa ametoa ulimi wake nje ukiwa na punje mbili za karafuu katikati yake.

Tafuna Punje mbili za karafuu asubuhi kabla ya kula kitu upate faida hizi kwa afya yako

Punje mbili tu za karafuu zinatosha kuupatia mwili wako virutubisho vyake muhimu kwa afya yako kama utazitumia punje hizo asubuhi na mapema au wakati tumboni kwako bado hujaweka kitu kingine chochote.

Ukifanya hivyo mara kwa mara virutubisho kwenye punje hizo za karafuu vinaweza kusaidia afya ya mwili wako kwenye mambo haya yafuatayo.

Ni msaada kama umevimbiwa.

Moja kati ya msaada wa karafuu ni kuongeza uzalishaji wa vimeng’enyo vya chakula tumboni.
Vimeng’enyo hivyo vinasaidia kuongeza umeng;enyaji wa chakula tumboni na kukuondolea dalili za kuvimbiwa kwa haraka.
Pia baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa karafuu inasaidia kudhibiti bakteria hatari tumboni wanaoweza kusababisha magonjwa mengine ya tumbo.

Inasaidia kuimarisha afya ya ini.

Virutubisho kwenye karafuu vinasaidia kuzikinga seli za ini dhidi ya kemikali hatari mwilini, na vinasaidia kuchochea uzalishaji wa seli mpya za ini na kusaidia kuongeza uwezo wa ini kusafisha sumu mwilini.

Inasaidia kudhibiti kiwango sukari kwenye damu.

Ni muhimu kwa wenye tatizo la kisukari, kwa kutafuta karafuu asubuhi au kabla ya kula kitu chochote inasaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu.
Inasaidia kuongeza uzalishaji wa homoni ya insulin mwilini na kuongeza ufyonzaji wa sukari kutoka kwenye damu kuingia kwenye seli za mwili kwa matumizi yake ya kawaida.

Inasaidia kuimarisha kinga ya mwili.

Virutubisho kwenye karafuu vitakusaidia kuimarisha kinga yako ya mwili na kukukinga na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza, hasa magonjwa kwenye mfumo wa hewa kama vile mafua, kifua na vidonda kwenye koo.
Pia karafuu inasaidia kudhibiti baadhi ya virusi hatari mwilini.

Inasaidia kuondoa kichefuchefu.

Unapotafuna punje za karafuu kuna baadhi ya vimeng’enywa vinazalishwa pindi tu virutubisho vya karafuu vinapochanganyika na mate.
Vimeng’enywa hivyo vinasaidia kuondoa hali hiyo ya kichefuchefu.

Ni tiba na kinga ya matatizo ya meno na kinywa.

Mbali na kukusaidia kutibu maumivu ya meno pia karafuu inasaidia kutibu na kukukinga na matatizo mengine ya kinywani kama vile ukungu kwenye meno, kuvimba fizi na fizi kutoa damu.

Inasaidia kuimarisha mifupa na kupunguza maumivu kwenye joints.

Wingi wa madini ya manganese kwenye karafuu unasaidia kuongeza ujazo kwenye mifupa na kuifanya kuwa imara, pia inasaidia kuimarisha tishu za mifupa hali ambayo inasaidia kupunguza maumivu kwenye viungio vya mwili au joints.

Inasaidia kuimarisha afya ya ubongo.

Kutokana na uwepo wa madini ya manganese kwa wingi kwenye karafuu inasaidia kuimarisha afya ya ubongo.
Inasaidia kuongeza uwezo wako wa kufikiri na kutunza kumbukumbu.

Ni kinga dhidi ya saratani.

Baadhi ya tafiti za maabara zimeonesha kuwa virutubisho kwenye karafuu vina msaada wa kudhibiti ukuaji wa baadhi ya seli za saratani mwilini.

Tiba ya vidonda vya tumbo.

Baadhi ya tafiti kwa wanyama zimeonesha kuwa virutubisho kwenye karafuu vina uwezo wa kudhibiti bakteria wa H.Pylori, bakteria ambao kwa asilimia kubwa husababisha vidonda vya tumbo.

Tafiti hizo bado zinahitaji tafiti nyingine zaidi kuthibitisha uwezo uwo wa karafuu kwa binadamu.

0
0
1