
Kabla ya kula kitunguu maji zingatia mambo haya
Tangawizi ni moja ya kiungo cha mizizi ya mti ambacho wengi tunakitumia kuongeza ladha ya chakula.
Pia tangawizi unaweza kuitumia kama tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya kwasababu ina virutubisho muhimu kwa afya ya binadamu.
Unaweza kuitumia tangawizi kwa tiba ya kichefuchefu na kutapika, tiba ya maumivu ya tumbo wakati wa hedhi kwa wanawake,
maumivu ya mifupa na viungio vya mwili, tiba ya kisukari na maumivu ya kichwa.
Kuna faida zingine nyingi za kutumia tangawizi kwa afya ya binadamu, link ipo kwenye description hapo chini kama utapenda kufahamu zaidi.
Kabla ya kutumia tangawizi ni vizuri ukazifahamu tahadhari hizi:
Kama utaitumia kwa kuitafuna hakikisha unatumia kiasi kidogo cha tangawizi kisichozidi gramu 1 kwa siku.
Ikiwa utaitumia kwa wingi tangawizi inaweza kusababisha kiungulia, kubeua, kuharisha, na matatizo mengine ya tumbo.
Ni vizuri kuitumia tangaizi kwa kuchanganya kenye chai, vinywaji au vyakula vingine ili kuepuka matumizi ya tangaizi kwa kiwango kikubwa.
Kwa wajawazito pia tangawizi inashauriwa kutumiwa kwa kuchanganya na vyakula vingine, pia unaweza kuitumia tangawizi kama tiba ya
kichefuchefu na kutapika kipindi cha ujauzito.
Tangawizi inaweza kuongeza hatari ya kuvuja damu nyingi, hivyo kuna baadhi ya wataalamu hawashauri matumizi ya
tangawizi siku chache kuelekea kujifungua au kufanyiwa upasuaji.
Ni muhimu kusitisha matumizi ya tangawizi wiki mbili kabla ya kwenda kufanyiwa upasuaji.
Kwa wamama wanaonyonyesha ni salama kutumia tangawizi kwa kuichanganya na vyakula vingine,
epuka matumizi ya tangawizi kwa wingi kwasababu hakuna tafiti za kutosha zinazoonesha usalama wa tangawizi kwa mama anayenyonyesha.
Matumizi ya tangawizi kwa wingi pia tafiti zinaonesha kuwa inaeza kuchochea matatizo ya moyo kwa wenye magonywa ya moyo.
Unaweza pia kusoma: